ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 5, 2018

DRC YAFUNGA MBUNGA YA WANYAMAPORI YA VIRUNGA BAADA MASHAMBULIZI

DRC yafunga mbunga ya wanyamapori ya Virunga baada ya mashambulizi


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kusitisha shughuli za utalii ndani ya Mbuga ya Wanyamapori ya Virunga hadi mwaka ujao kufuatia mashambulizi kadhaa na utekaji nyara ndani ya mbuga hiyo.
Shirika la kitaifa linaloshughulikia maswala ya utalii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ICCN limesema kuwa limesitisha Shughuli za Utalii ndani ya Mbuga ya wanyamapori ya Virunga hadi mwaka ujao.
Hatua ya kufunga Mbuga hii inakuja siku chache baada ya kushuhudiwa visa vya utekaji nyara katika hifadhi hiyo ambayo ni kivutio kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mei 11, 2018 watali wawili kutoka Uingereza walitekwa nyara, kabla ya kuachiwa huru baada ya jeshi la DRC, kuendesha operesheni maalumu ya kuwaokoa watu hao kutoka mikono ya watekaji nyara. Aidha mwanamke mmoja mlinzi wa mbuga hiyo aliuawa na watu wasiojulikana.


Awali Mbuga ya Wanyamapori ya Virunga ilifungwa kwa muda, na ilikua inatazamiwa kufunguliwa jana Jumatatu, amesema mkurugenzi wa mbuga hiyo katika taarifa yake.
Pasteur Cosma Wilungula wa ICCN amethibitisha kuwa kutekwa nyara watalii wawili na pia kuuawa kwa mmoja wa walinzi ndiyo sababu kuu ya kufungwa mbunga hiyo. Amesema kunafanyika mikakati ya kuboresha usalama katika mbuga hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.