ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 5, 2018

NEEMA MSIMU WA RAMADHAN RC MAKONDA AGAWA KONTENA LA TENDE KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA.

 NA ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea shehena ya Tende kutoka Taasisi ya Darul Irshaid Islamic kwa kushirikiana na Miraji Islamic Center Kama sehemu ya sadaka kwa waislamu katika *mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.* 

RC Makonda amesema tende hizo zitatolewa kwa vituo vya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu vilivyopo Jijini Dar es salaam. 

Aidha RC Makonda amewasihi kinadada kuheshimu imani za watu kwa *kujisitiri* na kuvaa nguo za heshima ili kuepuka kuharibia Swaumu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic center Bwana Arif Yusuph Abdulrahman amesema wameamua kutoa tende hizo Kama sehemu ya sadaka katika mwezi wa Ramadhan.

 Kutoa Sadaka (Sadaqa)
Yapo malipo makubwa kwa mwenye kutoa Sadaka ndani ya mwezi huu wa Rajabu. Wale ambao hawawezi kufunga wanaweza kutoa Sadaka kwa kuwapa masikini kila siku.



Kuhusu falsafa na hekima ya funga au saumu yamezungumzwa mengi ndani ya Qur’ani tukufu, Hadithi pamoja na kauli za maulamaa wa dini. Katika kubainisha hukumu ya kufaradhishwa na kuwajibishwa kufunga, Qur’ani tukufu imeitaja taqwa na uchaMungu kuwa moja ya hekima za kufaradhishwa amali hiyo tukufu. Aya ya 183 ya Suratul Baqarah inasema:

Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama walivyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha Mungu.

Funga ni moja ya amali bora kabisa za kumwezesha muumini kudhibiti ghariza za kihayawani na kuhuisha moyo wa uchaji Mungu ndani ya nafsi yake. Kama ilivyoelezwa katika Hadithi ni kwamba: “Funga ni ngao (ya Moto wa Jahannamu)”. Yaani mtu atanusurika na kuokoka na Moto wa Jahannamu kutokana na kufunga. Na sababu ni kuwa, kutokana na t’aa, ibada anazofanya mtu na kuzidhibiti na kuzidhoofisha hawaa na matamanio ya nafsi hatimaye huweza kumdhibiti na kumshinda shetani wa ndani na nje ya nafsi yake. 

Na ni kutokana na hayo ndipo Bwana Mtume Muhammad SAW akasema: “Ndani ya mwezi huu mashetani hufungwa pingu na minyororo, basi mwombeni Mwenyezi Mungu asiwasalitishe juu yenu”.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.