ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 18, 2018

BIA YA KILIMANJARO YAFANIKISHA NDOTO ZA WATANZANIA 10 KUONA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA 2018, URUSI


Baadhi ya washindi wakiwa na Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL,David Tarimo (wa pili kutoka kushoto).
Shamrashamra za hafla ya uzinduzi wa kuangalia mechi za kombe la Dunia jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika hafla hiyo

*Wengine waendelea kujishindia fedha taslimu shilingi milioni moja

Wakati mashindano ya soka ya kombe la dunia 2018 la FIFA, yameanza ,bia  rasmi ya kwanza ya Tanzania katika mashindano hayo ya Kilimanjaro Lager, kupitia promosheni  yake inayoendelea  imefanikisha ndoto za watanzania 10 kwenda nchini Urusi kushuhudia mechi za mashindano hayo makubwa ya soka dumiani mubashara.

Washindi  kupitia promosheni  ya bia ya Kilimanjaro ya Kombe la Dunia, iliyozinduliwa  mapema mwezi uliopita wako katika maandalizi ya safari kwenda Urusi mapema mwanzoni mwa wiki ijayo.

Baadhi ya washindi walipohojiwa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na safari hiyo walisema kwa furaha kuwa mwanzoni walikuwa hawaamini baada ya kupewa taarifa za ushindi wa droo za promosheni hiyo lakini hivi sasa baada ya kukabidhiwa tiketi zao wameamini safari ipo.

Charles John, mmoja wa washindi hao kutoka mkoani Geita,ameeleza kuwa anajisikia furaha kupata fursa kama hii ambayo alikuwa haitegemei,ameishukuru kampuni ya TBL kwa kuandaa promosheni kubwa kama hii ambayo imefanikisha ndoto za wateja wake kuona mechi za kombe la Dunia Live.

Mshindi mwingine, Leodgard Isaac,alisema kupata nafasi hii ni moja ya jambo ambalo limeleta furaha maishani mwake na kuongeza kuwa mbali na kuona mechi za kombe la Dunia Live pia anafurahi kuona kinywaji kutoka Tanzania cha  bia ya Kilimanjaro, kimetumika kuitangaza Tanzania katika  mashindano haya makubwa  ya mchezo wa soka duniani.

Naye Kaijage Kironde, mkazi wa Dar es Salaam,alisema ni mpenzi wa mchezo wa soka kwa miaka mingi,na amefurahi kupata  nafasi ya kushuhudia  mchezo wa kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro.

Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, alisema,promosheni inaendelea kwa washindi wa  fedha taslimu milioni moja kila wiki na muda wa maongezi inaendelea na katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki washindi 4 wamejishindia fedha, “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”, alisisitiza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.