ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 17, 2018

NGURUWE ALIYEITABIRIA MAKUBWA NIGERIA - 2018 FIFA WORLD CUP RUSSIA AUAWE.




HABARI- /- BBC SWAHILI

Nigeria walazwa 2-0 na Croatia, Denmark 1-0 Peru, Argentina 1-1 Iceland, Ufaransa 2-1 Australia

Messi ashindwa kufunga penalti dhidi ya Iceland, mchezaji ambaye babake ni Mtanzania Yusuf Poulsen afungia Denmark

Imekuwa siku nyingine ya masikitiko kwa Afrika baada ya mwakilishi mwingine Nigeria kulazwa 2-0 na Croatia katika mechi ya Kundi D.
Misri na Morocco walikuwa Ijumaa wamechapwa 1-0 na Uruguay na Iran.
Matumaini sasa ni kwa Tunisia watakaokutana na England Jumatatu saa tatu usiku na Senegal watakaokutana na Poland Jumanne saa kumi na mbili usiku.
Misri watakuwa tena uwanjani saa tatu usiku siku hiyo dhidi ya wenyeji Urusi.
Siku ilianza kwa mechi za Kundi C katika ya Ufaransa na Australia. Pande zote zilikabidhiwa penalti baada ya refa kushauriana na waamuzi wenzake upande wa teknolojia wa VAR.

Pande zote zilifunga penalti zao, lakini mwishowe Ufaransa iliilaza Australia 2-1 baada ya bao la Paul Pogba kuvuka mstari.
Aidha, kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia mwaka huu, Penalti tano zilitolewa huku mbili kati yao zikipotezwa na wachezaji katika muda wa kawaida wa mchezo.
Katika uwanja wa Spartak mjini Moscow, taifa ndogo la Iceland liliwashangaza wengi baada ya kujitetea dhidi ya Ajentina.
Lionel Messi alinyimwa bao la penalti na kipa wa Iceland Hannes Halldórsson ambaye aliishia kutuzwa mchezaji bora wa mechi. Refa kutoka Poland Szymon Marciniak aliipa Argentina penalti dakika ya 63 baada ya Maximiliano Meza kulazwa na Rurik Gislason.
Ingawa Aguero ailiiweka Argentina kifua mbele dakika ya 19, bao lake lilifutwa na Alfred Finnbogason dakika chache baadaye.
Mchuano huo ulifuatwa na ule wa Denmark na Peru ambapo Denmark ilijinyakulia ushindi kupitia mshambulizi mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen.
Licha ya kupoteza mechi na fursa ya kuongoza kupitia penalti, kikosi cha Peru kiliweka historia kwa kuliwakilisha taifa hilo katika kombe la dunia tangu 1982. Christian Cueva alipoteza mkwaju wake dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika. Shuti lake lilipaa angani.
Kocha wa Denmark Age Hareide amemtaja kipa wake Kasper Schmeichel na mabeki kwa kuchangia ushindi huo.
Siku iliisha na mechi ya Kundi D kati ya Croatia na Nigeria. Makosa ya mabeki yalipelekea Nigeria kulazwa 2-0 na kuninginia mkiani.
Timu hiyo imesalia na kibarua kigumu kwani ndio timu pekee bila alama lkatika kundi hilo

Muda wa ziada Croatia bado kifua mbele

Croatia 2-0 Nigeria
Mashabiki wa Nigeria wana matumaini makubwa lakini muda hauna huruma.
Zimeongezwa dakika 4 za zaida, lakini Croatia ndio inakaribia kuondoka na ushindi.

Kombe la - mikwaju ya penalti?

Penalti tano ndani ya siku moja.
Mechi za kombe la dunia leo zimekaribia kuvunja rekodi ya idadi ya Penalti kutolewa.
Mkwaju wa dakika chache zilizopita uliotiwa kimiani na Luka Modric ni wa tano kukabidhiwa timu.
Rekodi ya Kombe la dunia ni penalti sita ndani ya siku moja. Luka Modric amewafungia Croatia bao la pili, kupitia mkwaju wa penalti baada ya William Ekong kumuangusha Mario Mandzukic kwenye sanduku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.