Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu. |
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akibadilisha mawazo na baadhi ya viongozi walikuwa kwenye eneo la ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu. |
Na Fredy Mgunda,Ileje
HALMASHAURI ya wilaya ya Ileje
mkoani songwe imetumia zaidi ya shilingi milioni mia moja themanini katika ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za EPFR ambazo
hutolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi.
Akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa kukagua miradi hiyo,mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi alisema
kuwa jukumu la uongozi ni kuhakikisha kuwa pesa inayotolewa na serikali
inatumika kama ilivyokusudiwa na serikali kuu kwa faida ya sekta ya elimu.
“Serikali inatoa pesa nyingi
sana hivyo tusipo simamia vizuri pesa hizi zitapotea kitu ambacho Rais wetu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli hataki kabisa kusikia kuna
pesa ambayo haitumiki kama ilivyokusudiwa ndio maana nimeamua kuanza kukagua
miradi yote ambayo inatekelezwa katika halmashauri yetu” alisema Mnasi
Mnasi aliwaomba wananchi
kuchangia nguvu zao kuhakikisha shughuli za ujenzi wa madarasa na vituo vya
afya wanajitolea vilivyo ili kuendelea kufanya kazi sambamba na kasi ya
serikali ya awamu ya tano.
“Mimi binafsi nawaomba wananchi
wajitolee kufyatua tofali ,kuchota maji,kubeba mchanga na kusomba tofali ambazo
zinakuwa zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya ujenzi ambao utakuwa na faida
kwao na vizazi vijavyo” alisema Mnasi
Aidha Mnasi aliwapongeza
wananchi wa halmashuri ya Ileje kwa kuendelea kujitolea kufanya kazi kwa kuunga
mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya wamu ya tano ambayo imelenga kuleta
maendeleo kwa wananchi wake
“Mpaka sasa kuna asilimia kubwa
ambayo wananchi wamekuwa wakijitolea kufanya kazi za kimaendeleo ambazo
zinawahusu japo sio kwa asilimia kubwa kutokana na idadi kubwa ya wananchi
wanaoishi katika wialya hii hivyo nitoe wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza
kwenye maendeleo ili kuijenga ileje yetu mpya” alisema Mnasi
Mnasi alisema kuwa kipaumbele
cha halmashauri kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wanaboresha sekta ya elimu na
sekta ya afya ili kukuza maendeleo ya wilaya kwa kasi kubwa.
“Ujenzi unaendelea ni wa
madarasa ya shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu na kuhakikisha
wananchi wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao” alisema
Mnasi
Naomba nimalizie kwa kupongeza
serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Maguli kwa kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi
wanapata maendeleo kwa kuboresha sekta za elimu,miundombinu afya na n.k
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.