NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
Mkurugenzi mkuu wa hospital ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza Daktari Abel Makubi amebaini njama za muda mrefu dhidi ya hospitali hiyo zinazofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa wazalendo kwa kuwalaghai wagonjwa wanaokuja kupata matibabu kwenye hospitali hiyo na kuwahamishia hospitali zingine.
Ni hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza ambayo inahudumia wagonjwa mbalimbali wakiwemo wa ndani na nje ya mkoa huu, hivi karibuni katika hospitali hii kuwekuwepo na baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu ambao baadhi yao wamekua wakiwalaghai wagonjwa .
Akizungumza na vyombo vya habari mkoani Mwanza Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Bugando Daktari Abel Makubi hapa anaeleza baadhi ya hujuma juu ya hospitali hiyo.
Mbali na Vitendo hivyo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watumishi kwa wagonjwa vimekua vikiathiri huduma hospitalini hapo.
Dr Frank Masasi ni mkurugenzi wa utawala na utumishi hospitlini hapo huku Dr Makubi akawatoa hofu wagonjwa wa kansa na kuwaahidi huduma hiyo itapatikana huspitalini hapo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.