Mgeni
Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika
katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini
Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Mgeni
Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika
katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini
Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Baadhi
ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa
makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati
akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba
24, 2017.
Baadhi
ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa
makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati
akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba
24, 2017.
Mgeni
Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia mada kuhusu
Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali
vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo
Novemba 24, 2017.
Mgeni
Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika
katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini
Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Baadhi
ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa
makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati
akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba
24, 2017.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Wanahabari
kote nchini wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Kilimo ili
ifanikiwe katika jitihada zake za kuhakikisha kwamba Tanzania inafikia
lengo la Azimio la Maputo la kumwezesha
mkulima kufikia matumizi ya kilo 50 za virutubisho kwa hekta badala ya
hali ya sasa ambapo anatumia kilo 19 tu au asilimia 38 ya lengo la
Maputo.
Mwito
huo umetolewa Leo Novemba 24, 2017 na Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mkutano huo ulikuwa na dhamira ya kujifunza na kuongeza uelewa kwa wahariri juu ya Mifumo mipya iliyoanzishwa na Serikali kuhusu Uagizaji wa Mbolea kwa Pamoja (Bulk Procurement System - BPS) na Usimamizi wa bei Elekezi ya Mbolea (Indicative Pricing Structure - IPS) kwa
lengo la kumwezesha Mkulima kupata mbolea bora na kwa bei nafuu ili
kuongeza matumizi ya mbolea yatakayo chochea, ongezeko la uzalishaji
nchini ili kukidhi mahitaji ya familia na kuuza ziada ndani na nje ya
nchi.
Mhe
Mwanjelwa alisema Wizara ya Kilimo imebaini kuwa wafanyabiashara wadogo
wa mbolea wanaokiuka bei elekezi kutokana na wafanyabiashara wakubwa
kuwauzia wafanyabiashara hao wadogo kwa bei elekezi ya rejereja badala
ya bei ya jumla licha ya kufahamu kuwa wanatakiwa kugawana faida na
wauzaji wa rejareja lakini bado wanakiuka taratibu za kisheria hivyo
aliwasihi kuacha tabia hiyo ili mawakala wauze kwa rejareja na kwa bei
elekezi bila kuathiri biashara zao.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ina Mkakati wa kuongeza
matumizi ya mbolea ambao umekuwa na umuhimu wa pekee hasa ikizingatiwa
kwamba imeweka lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati
unaoendeshwa kwa viwanda.
Alisema
Kwa sehemu kubwa, viwanda hivyo vitategemea malighafi itokanayo na
mazao ya kilimo. Hivyo ili, kufikia lengo hilo, lazima kila mmoja
kutumia nafasi yake kuhakikisha kwamba tija itokanayo na Kilimo
inaongezeka kwani Mbolea ni moja ya vichocheo vikubwa.
“Pamekuwepo na Mifumo mbalimbali iliyoanzishwa kwa lengo la kumsaidia Mkulima
kupata mbolea za kutosha ili aongeze tija na uzalishaji katika kilimo
ambayo ni pamoja na ruzuku ya usafirishaji ili kuwezesha mbolea kuuzwa
kwa bei moja nchi nzima (Pan Territorial Prices). Baadae
ulifuata Mfumo wa wauzaji kulipwa sehemu ya bei na hivyo mbolea kuuzwa
kwa bei chini kuliko bei ya Soko. Sambamba na Mfumo huo, kulikuwa na
jitihada za kutengeneza mbolea hapa nchini ili kuepuka gharama kubwa za
uagizaji” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema
taarifa zinabainisha kuwa Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Mwanza na
Geita wafanyabiashara hufungua mifuko na kuuza mbolea ya kupandia (DAP)
kwa Tshs 2,000/= kwa kilo ili wapate Tshs 100,000/= kwa mfuko wa kilo 50
badala ya bei elekezi ya Tshs 51,000 – 56,000/=.
Aidha,
Mbolea ya kukuzia (Urea) wanaiuza kwa Tshs 1,500/= kwa kilo ili wapate
Tshs 75,000/= kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya Tshs 41,000 –
45,000/=. Pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora kwa
kufunguliwa na kuachwa wazi, wafanyabiashara hawa wanawaingizia wakulima
hasara kubwa ya mavuno.
Naibu
Waziri Mhe Mwanjelwa alisisitiza, “Ofisi yangu ina taarifa kwamba
baadhi ya wafanyabiashara wanatunza mbolea bila kuzingatia viwango
vilivyowekwa na TFRA. Haya ni makosa mabubwa sana kisheria kwani
yanasababisha mbolea kumfikia mkulima ikiwa imepungua ubora au
kuharibika kabisa na hivyo kumfanya mkulima asipate tija inayotokana na
matumizi ya mbolea. Huu ni uhujumu mkubwa sana wa uchumi wa Mkulima
pamoja na Taifa kwa ujumla”
Mbolea
ni kemikali ambayo virutubisho vyake huyeyukia hewani ikiachwa wazi kwa
muda mrefu. Kwa maana nyingine, kitendo cha kufungua mfuko wa mbolea
hufanya virutubisho (Nutrients) kuanza kupotea mara tu
vinapokutana na hewa. Hivyo kinachobaki kwenye mfuko ni makapi yasiyo na
manufaa katika kuongeza uzalishaji wa mazao. Aidha, mbolea ya kupima
inaweza ikageuka sumu kwa mimea na hata udongo na hivyo kufanya usifae
tena kwa matumizi ya kilimo.
Mkutano
huo wa Naibu Waziri wa Kilimo na wahariri wa vyombo vya habari nchini
ni mwanzo wa mahusiano chanya baina ya Waandishi wa habari na Wizara ya
kilimo ili kuinua sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono kwa vitendo
juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli katika kuimarisha uuchumi wa Wananchi kupitia kilimo ambao ni
uti wa mgongo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.