Mapungufu yaliyoko katika sheria ya elimu ya mwaka 1978
yanadaiwa kuchangia kumkosesha haki mtoto wa kike pale anapoolewa
kutokana na sheria hiyo kumtambua mtoto kuwa ni yule aliye katika shule
ya msingi pekee.
Akizindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia katika mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi mkoani Mwamwa ALLY MKALIPA amesema ni vigumu kuchukua hatua
pale mwanafunzi wa sekondari anapopata ujauzito au kuolewa hivyo
ameshauri kubadilishwa kwa sheria hiyo.
Mimba za utotoni zimeendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa mtoto wa kike katika kutimiza ndoto ya kupata elimu.
Mkoa wa mwanza ni miongoni mwa mikoa nchini inayokabiliwa na ongezeko la mimba za utotoni.
Katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya ziwa,baadhi ya changamoto
zinazochangia ongezeko la mimba miongoni mwa wanafunzi zikabainishwa.
Baadhi ya watendaji wa kata wakaelezea matatizo yanayochangia ongezeko la mimba za utotoni kwenye maeneo yao.
Akizindua maadhimisho hayo jijini mwanza,mrakibu mwandamizi
wa polisi mkoani mwanza ALLY MKALIPA akashauri kubadilishwa kwa sheria
ya elimu.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia mwaka huu ni funguka pinga ukatili wa kijinsia elimu salama kwa
wote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.