ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 27, 2017

WAKEZAJI WAMIMINIKA JIJINI MWANZA

 JOHN MONGELA ,Mkuu wa mkoa wa mwanza akimkabidhi YE DONGSON – Kiongozi wa Ujumbe kutoa China. zawadi mgeni huyo alie ambata na jopo la watu kumi na moja kwaajii ya kufanya mazungumzo ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda mkoani Mwanza..
  JOHN MONGELA ,Mkuu wa mkoa wa mwanza kushoto akikabidhiwa zawadi na mgeni wake YE DONGSON – Kiongozi wa Ujumbe kutoa China. mgeni huyo alie ambata na jopo la watu kumi na moja kwaajii ya kufanya mazungumzo ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda mkoani Mwanza
 Wakiagana.
 Aksante sana.
Picha ya pamoja.


Wawekezaji kutoka China wamewasili nchini kutafuta fursa za uwekezaji


PICHA NA HABARI: ZEPHANIA MANDIA
WA GSENGO BLOG

Serikali ya Taifa la China kupitia ujumbe wa watu kumi na moja wa Rais wa Taifa hilo Xi Jing Ping, imeahidi kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda nchini Tanzania, ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano zinazolenga kuimarisha uchumi kuelekea mwaka 2025.

Kauli mbiu ya Tanzania ni uchumi wa viwanda ambapo kwa mpango huo mkakati, ujumbe wa Rais wa China uliowasili Jijini Mwanza ukitokea nchini Rwanda, ukatumia mkakati huo kuihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa China itakuwa mstari wa mbele kuwekeza hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo baada ya kukamilisha ziara ya kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani Mwanza, kiongozi wa ujumbe huo kutoka Jimbo la Henan Ye Dongson, amesema kuwa  mazingira ya Tanzania yamewashawishi kuendelea kuwekeza katika sekta ya viwanda.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa idara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa China Bi. Song Liping, Naibu mkuu wa idara hiyo Chen Guociang, amesema mapendekezo ya ujumbe huo yatawasilishwa katika Serikali ya China, ili kuanza uwekezaji.

Mwenyeji wa ujumbe huo mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela, amesema kuwa Serikali bado inaendelea kukaribisha wawekezaji kuja kutafuta fursa za kuwekeza hapa nchini, ili kuliwezesha Taifa kutimiza hazima ya Tanzania ya Uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.