ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 22, 2017

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 102 KWA VIKUNDI 49 VYA WAJASIRIAMALI

 Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakiwa  katika picha ya  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika  kuendeshea shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mkuu wa Wilaya Kisarawe Happiness  Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi vya wajasiriamali kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa kuwawezesha kiuchimi.

 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda akizungumza jambo katika halfa fupi ya vikundi vya wajasiriamali.

 Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi vya wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)


NA VICTOR  MASANGU, KISARAWE


HALMASHAURI YA wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono  juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa vikundi vya wajasiriamali vipatavyo 49  vya wakinamama,vijana  pamoja na walemavu kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao  mbali mbali za biashara mbali mbali  ikiwemo  na kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi katika kujenga  viwanda vidogo vidogo.


Akizungumza katika halfa fupi ya kukabidhi  hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama  alisema kwamba fedha hizo za mikopo  zimetolewa kwa vikundi hivyo kutokea kata zote 17 ambapo zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuweza kukuza uchumi wa  nchi  kutokana na kuweza kuwapa fursa wajarisiamali hao kupania wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha viwanda vingine vidogo vidogo  ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa ajira mpya na kupunguza wimbi la umasikini.


“Kwa kweli sisi kama halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka mipango madhubuti katika kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa kutumia fedha zetu ambazo zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani, hivyo vikundi hiivi ni moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile asilimia 10 iliyotengwa inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ameviasa vikundi vyote vilivyopata mkopo huo  hususan kwa  wakinamama kuachana  kabisa na vitendo vya  kutumia fedha hizo vibaya kwa shughuli ambazo hazina manufaa yoyote kwa jamii, kama vile kuwachezesha  watoto  wao ngoma wakati wa kufunga shule   pamoja na kununulia madela kitu ambacho amekilaani vikali.


Aidha Seneda alisema kuwa malengo ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wananchi wake wanawezeshwa kwa namna mbali mbali ikiwemo kuwapatia mikopo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kukuza biashara zao pamoja na wengine kufanya biashara zao ndondogo amabzo zitaweza kuwapatia kipato na kujikwamua kiuchumi.


“Jamani mimi kama kiongozi wenu napenda kuwaasa wale wote mlionufaika na mkopo huu, kuhakikisha mnazitumia vizuri fedha hizi hasa kwa upande wa wakinamama ambao wamekuwa na tabia pindi wanapotata pesa wanazitumia katika matumizi mengine ya kununulia madela kwa ajili ya sare pamoja shughuli nyingine kama vile kuwacheza ngoma watoto wao hii tabia kwa kweli sipendi kuiona katika Wilaya yangu,”alisema Seneda.


Nao baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na mkopo wa fedha hizo   akiwemo  Monica Muhoza ambaye ni mlemavu wa miguu, Faudhia Kasikasi, pamoja na  Gudluck Akyoo  wameshukuru uongozi mzima wa halmashauri ya Kisarawe na kusema kuwa fedha hizo  walizopatiwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao  kwani zitaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi pamoja na kujikimu kimaisha na kuendesha familia zao.


VIKUNDI hivyo vya wajasiriamali 49 kutoka kata 17 za Wilayani Kisarawe zimewahusiha wakinamama, vijana, pamoja na makundi vya walemavu ambapo vimepata mkopo wa fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 102 ikiwa ni makusanyo ya mapato ya fedha za ndani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.