ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 9, 2017

JPM AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WATEULE.

Picha na Azam Two.
Oktoba 7 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mbili, kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo. Hatimae leo Rais huyo amewaapisha Mawaziri hao.

Rais Magufuli amewaapisha Mawaziri hao leo, Ikulu jijini Dar es salaam ambapo Mawaziri wote wameapa kiapo cha uaminifu.

Ambapo mara tu baada ya kuanza, Rais Magufuli alianza kwa kumuapisha Angella Kairuki kuwa Waziri wa Madini,

Hii ni orodha ya Mawaziri hao
1.Wizara ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.
Waziri – George Huruma Mkuchik

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Kangi Lugola

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Jenista Mhagama
Naibu Waziri – Anthony Peter Mavunde
Naibu Waziri Walemavu – Stela Alex Likupa

4.Wizara ya Kilimo
Waziri – Charles John Tizeba
Naibu Waziri – Mary Mwanjelwa

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri – Makame Mbarawa
Naibu Waziri – Atashasta Nditiye
Naibu Wziri – Elias John Kwandikwa

6.Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Dr Philip Mpango
Naibu Waziri – Dr Ashatu Kijaji

7.Wizara ya Nishati
Waziri – Medrad Matogoro Kalemani
Naibu Waziri – Subira Hamisi Mgalu

8. Wizara ya Madini
Wairi – Angela Kairuki
Naibu Waziri – Haroon Nyongo

9. Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri – Palamagamba Kabudi

10. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Agustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt Susan Kolimba

11 .Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Dr Hussein Mwinyi

12. Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri – Hamad Masauni

13. Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Waziri – William Lukuvi
Naibu Waziri – Angelina Mabula

14. Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri – Hamisi Kigwangala
Naibu Waziri – Ngailonga Josephat

15. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Waziri – Charles Mwijage
Naibu Waziri – Stella Manyanya

16. Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Joyce Ndalichako
Naibu Waziri – William Ole Nasha

17 .Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Ummy Mwalimu
Naibu Waziri – Faustine Ndugulile

18. Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Dr . Harrison Mwakyembe
Naibu Waziri – Juliana Shonza

19. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Isack Kamwelwe
Naibu Waziri – .Juma Hamidu Aweso

20. Mifugo na Uvuvi
Waziri – Luhaga Mpina
Naibu Waziri – Abdallah Ulega

21. Wizara ya TAMISEMI
Waziri – Suleiman Jafo

Baada ya kila mmoja kuapa, Mawaziri na manaibu waziri wote kwa pamoja wamekula kiapo cha maadili ya utumishi wa umma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.