Allen Komba, Mfanyakazi wa Kampuni ya
masuala ya Ulinzi ya Insight (Zamani Warrior Security) akipokea zawadi kutoka
kwa Jacqui Sugden akiwa kama mmoja wa wafanyakazi aliyeitumikia kampuni hiyo
tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007. Zawadi hiyo ilitolewa wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya
Insight ambayo ni Kampuni inayoaminika zaidi kwenye masuala ya ulinzi na
Usalama Afrika Mashariki na Kati, katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika
katika hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.
Oktoba
2017, Dar es Salaam: Kampuni ya WS Insight ambayo hapo awali ilijulikana kama Warrior
Security jana usiku iliandaa chakula cha jioni katika hafla ya kuadhimisha
muongo mmoja (miaka10) wa mafanikio, ikiwa ni miongoni mwa kampuni inayoaminika
katika utoaji wa huduma bora za ulinzi na usalama ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati.
Tukio hilo la
chakula cha jioni lilifanyika jana usiku katika Hoteli ya Sea Cliff na liliwakutanisha
zaidi ya wageni 100 kutoka katika sekta mbalimbali ambao waliburudishwa vilivyo
na mchekeshaji mahiri kutoka Kenya, Eric Omondi. Pia kulikuwapo na zawadi kwa
wafanyakazi ambao wameitumikia Kampuni hiyo kwa takribani miaka 10 sasa.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji na mmoja wa waanzilishi wa WS Insight, Tony Sugden alisema, “Baada
ya kutimiza miaka 10, ninajivunia kusema kwamba hii ni kampuni yetu. Kampuni
ilianza kufanya shughuli zake mkoani Arusha mwaka 2006 ambapo kwa sasa imeajiri
watu 1,500 kwa Tanzania pekee na ina jumla ya wafanyakazi 7,000 kwa nchi tano
ambazo tunatoa huduma.”
“Ws Insight ilianzishwa kwa lengo la kutengeneza Mazingira
salama ya kuwawezesha watu na biashara kuwa salama. Hilo ndilo jambo ambalo linatufanya
kila wakati kufikiria majibu wanayohitaji wateja wetu na tunatimiza hayo yote
kwa kufanya kazi zetu kwa kuzingatia uzoefu na ujuzi jambo ambalo linaongeza
ufanisi katika upatikanaji wa taarifa kila wakati. Hakuna yeyote anayeweza
kujilinganisha nasi kwa ufuatiliaji.”
Kampuni yetu
iliyoanzishwa Tanzania, imefanikiwa kujitanua hadi Sudan Kusini mwaka 2008, pia
nchini DRC mwaka 2011. Zambia ilifika mwaka 2013 na Kenya mwaka 2014 huku
tukibadili jina kutoka Warrior Security hadi kuwa WS Insight mwezi Machi mwaka
huu. Kampuni ya Insight Group kwa sasa ina mapato ya Dola za Marekani milioni
35 kwa mwaka.
Wateja wetu
ni pamoja na Tier One Mining, Oil & Gas, UN, Mashirikia yasiyo ya
kiserikali (NGOs), Serikali na taasisi za kibiashara ambazo zipo katika mazingira
magumu duniani.
Mambo ya muhimu kwa wahariri
Kuhusu WS INSIGHT
WS Insight (Zamani Warrior Security) ni kampuni ambayo
imejikita kwenye utendaji kazi (ikiwa na mapato ya Dola 35 milioni huku ikiwa
imeajiri zaidi ya wafanyakazi 7,000). Pia ina uzoefu wa miaka 10 ya utoaji
huduma zake kwa kiwango cha juu kwa wateja wetu barani Afrika zikiwamo nchi za
DRC, Sudan Kusini, Zambia, Kenya na Tanzania. WS Insight imekuwa ikifanya kazi
kaztika maeneo ambayo inayafahamu vyema katika Afrika Mashariki na Kati
ikihudumia wateja wakiwemo Tier One Mining, Oil & Gas, US State Department,
USAID, UN, ofisi za kidiplomasia, asasi za kimataifa, pamoja na taasisi
mbalimbali za kibiashara.
Kampuni
ilianza ikiwa na Tony Sugden na Ashton Towlr na Mkugenzi wa Tanzania akiwa Matt
Merrick.
Wasifu wa Tony Sugden –Mkuruenzi Mtendaji na
Ofisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni (Group)
Ni miongoni
mwa waanzilisi wa Warrior Security mwaka 2006. Tony amekuwa na uzoefu kwa zaidi
ya miaka 15 kwenye biashara ya ulinzi kwa ukanda wote wa Afrika Mashariki na
Afrika na Kati. Amekuwa akiongoza zaidi ya watu 5,000 na kuendesha programu za
mafunzo, hatua mbalimbali na mifumo mikubwa na midogo kwa wateja wakiwamo Idara
ya Ikulu ya Marekani, Taasisi za UN, mashirika ya kibiashara na pia ya watu
binafsi.
Wasifu wa Ashton Towler biography –Mkurugenzi na Mkuu wa Fedha
Ni
mwanzilishi wa Warrior Security mwaka 2006. Ashton ni mwanachama wa Taasisi ya
Chartered Accountants nchini Uingereza na Wales. Ashton amepata mafunzo ya
kompyuta na kupata shahada ya kompyuta daraja la la kwanza la juu (Hons) kutoka
Chuo Kikuu cha Manchester. Baada ya kuhitimu Ashton alifuzu kuwa mhasibu cheti
cha taasisi hiyo ya juu ya uhasibu na kufanya kazi na Arthur Andersen jijini
London na baadaye akajiunga na CDC Group ambapo alitekeleza majukumu mbalimbali
ya uwekezaji kwa miaka miatano ambapo alifanikiwa kufanya uwekezaji katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika Magharibi.
Ashton amepata uzoezfu mkubwa katika asekta
mbalimbali na kwenye mashirika mbalimbali
na kukuza mipango ya maendeleo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.