ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 3, 2017

HALI YA TAHARUKI YATANDA KWA WANANCHI BAADA YA KUKUTA MZOGA WA KUKU UMEVISHWA SANDA HUKU UKIWA NA MADAWA YA KIASILI

Mzoga wa kuku ambaye amefungwa na sanda kwa maelezo ya wananchi ambao walikuwa Nje ya Nyumba ya Bw Emmanuel Kabodi ambapo ndipo tukio hilo limetokea linalo husishwa  na imani za kishirikina.
Mama Mwenye Nyumba ambapo tukio hilo limetokea Bi,Scolastica Nicodemo  akizungumza na moja kati ya viongozi wa dini wakati alipofika kwenye familia hiyo kuona tukio hilo la kusitajabisha.
Baadhi ya wananchi wakishangaa jambo ambalo limetokea katika mtaa wa 14 kambarage.
Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye Nyumba hiyo.
Baadhi ya watu wakishangaa tukio hilo la kusitajabisha.

PICHA NA JOEL MADUKA 


Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala Wilaya na Mkoa wa Geita wamejikuta wakipigwa na Butwaa  baada ya kukuta mzoga  wa kuku  ukiwa  umevishwa sanda  kwenye familia ya Emmanuel  Kabodi.

Mama wa familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa   wakati  akifanya usafi  aliona  nyuma  ya geti  kuna kitu kimefungwa na shuka  jeupe na alipojaribu  kukiangalia aligundua  ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.

Askofu wa kanisa la  TMRC Mkoani Geita Stephano Saguda  ameihasa jamii kuachana na maswala  yanasosadikiwa kuwa ni ya kishirikina  kwani vitendo hivyo havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .

Mjumbe wa Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata,amesema  tukio hilo ni mara ya pili kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la kufukuliwa  kwa mtoto  na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya vitendo hivyo kuachana  navyo mara moja  kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo hawataweza kumvumilia.

Wananchi ambao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho kutokana na matukio hayo kuendelea kujitokeza mara kwa mara.

Mtaa  wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na vitendo vinavyosadikiwa ni vya Imani za kishirikiana vya mara kwa mara na  kusababisha  hofu kubwa kwa watu ambao wanaishi maeneo hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.