Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli (kushoto) akiteta jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyeta. |
Kenya na Tanzania zitafanya mazungumzo mwezi Novemba ili kuimarisha biashara kati ya pande hizo mbili.
Katibu mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na ushirikiano
nchini Kenya Chris Kiptoo amesema mjini Nairobi kuwa, nchi hizo mbili
zina wasiwasi baada ya kushuka kiwango cha biashara baina yao tangu
mwaka 2015.Amesema pande mbili zimekubaliana kukutana mjini Mombasa kwa ajili ya kutafuta njia ya kuondoa vizuizi vya ushuru ambavyo vinasababisha kushuka kwa biashara.
Habari hiyo inatolewa wiki moja baada ya Kenya na Tanzania kufanya mazungumzo ya siku tatu mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Matrela yakiwa na mizigo.
Mazungumzo hayo yalilenga kutatua vizuizui vya biashara ya bidhaa kama vile maziwa, tumbako, gesi na nyama.
Kumekuwepo na mvutano wa muda mrefu wa kibiasahra kati ya Kenya na
Tanzania jambo ambalo limepelekea kudhoofika jitihada za kuleta
ushirikiano zaidi baina ya nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.