NA VICTOR MASANGU, PWANI
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri
wa Nchi kavu na
majini (SUMATRA) Mkoa wa Pwani hatimaye umefanikiwa kumaliza na
kusuluhisha sakata la mgomo uliofanyika jana
kwa madereva wa mabasi madogo ya
daladala yanayofanya safari zake kuanzia katika stendi ya mbezi kuelekea
katika maeneo mbali mbali ya Wilayani Kibaha hadi Msata Wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusina na sakata hilo mara baada ya
kumalizika kwa kikao maalumu baina yao na uongozi wa madereva wa mabasi madogo Afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Pwani Omary
Ayoub amesema kuwa mgomo huo ambao ulitokea
siku ya jana ulidumu kwa kipindi cha zaidi ya masaa saba na kusababisha
usumbufu mkubwa kwa abiria waliokuwa wanahitaji huduma ya usafiri.
Ayoub alibainisha kwamba wameweza kubaini kuwepo kwa ongezeko la nauli
kiholela kwa abiria hao baada ya kufanya zoezi la kugagua magari zaidi ya 100 na
kukuta abiria wanalipishwa kiwango kikubwa kinyume kabisa na taratibu,na
kuongeza suala hilo kwa sasa wameshakutana na viongozi wa mabasi hayo na
kukubaliana kiwango halali ambacho
kinatakiwa kutumika.
“Ni kweli kulikuwa na hali ya sintofahamu baada ya baadhi ya
madereva wa mabasi madogo ya abiria yanayoanzia luti zake katika kituo cha
mbezi Jijini Dar es Salaam kuelekea maeneo ya Kibaha mpaka msata kugoma kupakia
abiria kutokana na kugomea nauli ambayo imepagwa na ipo kihalali kabisa ila kwa
sasa nashukuru tumekaa na viongozi wao wa mabasi na tumeshalimaza na viwango
vyetu tulivyovipanga ndi vitatumika na sio vinginevyo,”alisema Ayoub.
Ayoub alifafanua zaidi kuhusina na tukio hilo alisema kuwa
madereva hao waliamua kugomea kwa makusudi viwango vya nauli kilichopangwa na
mamlaka hiyo na kujiamulia kujipangia bei yao mwenyewe na kuwatoza abiria
wanaotokea mbezi kuelekea Kibaha kiwango
kikubwa tofauti na kile ambacho kilitolewa hapo awali kitu ambacho ni kinyume
kabisa na taratibu.
“Huu mgomo sisi kama Sumatra kwa kushirikiana na jesho la polis
tulifanya zoezi la kukagua magari kwa lengo la kuboresha huduma ya usafiri na
ndipo tulipobaini kuna makosa ambayo
yanafanywa ya kuwatoza nauli kubwa abiria tofauti na umbali wanayokwenda, na
kitu kikubw amfano nauli ya kutokea mbezi kwenda maili moja kibaha inatakiwa
kulipia shilingi mia tano lakini cha kushangaza wao walikuwa wanalipisha
shilingi mia nane yani wamepandisha mia tatu nzima,”alisema.
Kwa upande wake
Jaheka Mdami Mwenyekiti wa madereva
wa mabasi madogo yanaofanya safari zake kutokea kituo cha Mbezi Jijini Dar es
Salaa kuelekea Kibaha amesema kwamba kwa sasa mgomo huo wa madereva umeshamalizika ambapo wameshakubaliana na
uongozi wa Sumatra kutumia viwango vya nauli ambavyo vimeelekwezwa kwa mujibu
wa sheria.
Naye Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Pwani Salum
Molimoli amesema kuwa wameamua kufanya oparesheni kwa ajili ya kukagua magari
mabovu kwa lengo la kuweza kupunguza wimbi la ajali pamoja na kutoa elimu kwa
madereva kuhusiana na madhara yatokanaayo na unywaji wa pombe wakati
wakiendesha vyombo za moto .
Kamanda Molimoli alisema kwamba kwa sasa wana mikakati
kabambe ya kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara ambao utaweza
kusaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia ajali za barabarani ambazo wakati mwingine
zinatokana na uzembe wa madereva wenyewe.
“Katika kuhakikisha kwamba ajali za barabarani katika Mkoa
wetu wa Pwani zinapungua kabisa tumejipanfa kufanya ugaguzi wa mara kwa mara
ili kuweza kubaini magari ambayo ni mabovu na yanatembea barabarani, na kitu
kingine ni kuweka mipango ya kuweza kutoe elimu zaidi ambayo iataweza
kuwasaidia madereva pindi wanapokuwa njiani,”alisema Molimoli.
Mamlaka ua Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) kwa
kushirikiana na jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanikiwa kuyakamata magari zaidi ya 100 kutokana na
makosa mbali mbali ikiwemo kuvunja sheria ya kutozingatia sheria za
barabarani, kutokufunga mikanda, kuendesha magari mabovu pamoja na kuzidisha kiwango cha nauli kwa abiria.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.