ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 13, 2017

WAFANYABIASHARA NJOMBE WAGOMA.



Wafanyabiashara katika mji wa Makambako Mkoani Njombe wamefunga maduka na soko kuu wakiishinikiza Serikali kigawa Bure Mashine za kielektronic za kutolea Risiti za EFD.

Zaidi ya Maduka 90 yameonekana Kufungwa huku maeneo yaliyoonekana Kuathirika Zaidi ni Stand ya Zamani, soko kuu na Stand Mpya.

Wakizungumzia Uamuzi huo wafanyabiashara hao wanasema hawapingi Mpango wa serikali wa kutumia mashine hizo bali wanachokitaka ni Serikali kuwapa Mashine hizo Bure kama ilivyofanya Jijini Dar Es Salaam.

Pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kutekeleza agizo hilo la kununua mashine, Miongoni mwao wamelalamikia kutapeliwa na Makpuni yaliyoingia Mkataba wa kusambaza mashine hizo. 
Mgomo huo wa wafanyabiashara umemfanya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufika Mjini Humo ili kufanya mazungumzo ambapo wafanyabiashara hao wameonekana kushikilia msimamo wao wa kutaka kupewa bure mashine hizo.

Katika mazungumzo Hayo Olesendeka amesema viongozi wa wafanyabiashara wanatakiwa kuwa Daraja kati ya wafanyabiashara na Serikali.

Katika maagizo yake amesema hatovumilia mtu au watu watakaoonekana kutishia kufanya maandamano katika mkoa wake.

Mpaka muda huu mjadala baina ya wafanyabiashara na mamlaka za serikali bado unaendelea ili kujua nini muafaka wake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.