Cristiano Ronaldo alifunga bao
lakini baadaye akafukuzwa uwanjani huku Real Madrid wakilaza Barcelona
3-1 katika Super Cup ya Uhispania, mechi ya mkondo wa kwanza.
Ronaldo, aliyeingia kama nguvu mpya alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga.
Alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake kusherehekea.
Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kujiangusha na akafukuzwa uwanjani.
Marco Asensio alifunga la tatu.
Ronaldo aliamini kwamba alifaa kupewa penalti baada yake kuanguka alipokabiliwa na Samuel Umtiti, na alionekana kumsukuma refa baada yake kuoneshwa kadi nyekundu.
Ronaldo alikaa dakika 24 pekee uwanjani.
Barcelona walionekana kutatizika bila Neymar ambaye alihamia Paris Saint Germain kwa rekodi ya dunia ya £200m.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.