ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 14, 2017

"SASA NI ELIMU TU" ASEMA RIDHIWAN JK

 Mbunge wa Chalinze ameendelea kuhimiza maendeleo na Siku ya Tarehe 12 August 2017 alijikita kwenye sekta muhimu ya Elimu.

Safari ilianza jimboni humo akiwa ameambatana na Balozi wa Pakistan nchini Bw. Amir Muhammad Khan (juu pichani katikati) ambaye pia aliongozana na wanajumuiya ya Wapakistan wanaishi na kufanya Biashara Nchini Tanzania wamekabishi kwa Mbunge wa Chalinze Shule ya Msingi ya Utete ambayo wananchi wamekubali kuipa jina la Pakistan Mtete katika kuenzi juhudi kubwa zinazofanywa na raia hao wa Pakistan wanaoishi Tanzania.

"Tunayo safari kuelekea Tanzania ya Viwanda, na bila kuimarisha mfumo wetu wa utoaji elimu hatuwezi kutoa vijana watakaoingia katika ushindani wa ajira unaotakiwa"

"Mbali na hilo ushindani wa kiuchumi na biashara uliopo Afrika Mashariki nao una tusukuma kuuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa vijana wetu ili wawe bora na madhubuti katika kukabiliana na mapinduzi yaliyopo" alisema Mhe. Ridhiwan kisha akaongeza.

"Kama tunania ya dhati kumsaidia Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli na sera iliyopo sasa lazima tushiriki pamoja kupata msingi ambao ni vijana wenye ujuzi wa kufanya kazi,  hii ni changamo"

Ngao ya heshima kutambua mchango wa maendeleo.
Mbele ya geti kuu.
"Sasa na tuzindue kwa kukata utepe"
  Balozi wa Pakistan, Bw. Amir Muhammad Khan  pia alipata fursa ya kuhutubia wageni waalikwa ambapo alieleza nia ya wazi ya Serikali ya Pakistan kuzidi kukuza ushirikiano wa kiplomasia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba, licha serikali yake kusapoti elimu pia Pakistan imekuwa ikishiriana na Tanzania katika  sekta ya usafiri  upande wa reli, taasisi za kifedha na ushirikiano katika masuala ya ulizi na usalama. 
 
Washirika wa Maendeleo Chalinze. #HapaKaziTu #ChalinzeKaziTu #MagufuliKaziTu #MapinduZiChalinze

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.