Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano
makubwa wakitaka Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo aliyeko London
nchini Uingereza arejee nyumbani na kujiuzulu.
Wanigeria walifanya maandamano hao yaliyoitishwa na jumuiya za
kiraia wakipinga kitendo cha rais wa nchi hiyo kuendelea kuishi nje ya
nchi kwa kipindi cha miezi mitatu. Buhari anayesumbuliwa na maradhi
ambayo hayajatangazwa rasmi, amelazwa katika hosptali moja mjini London.Wakati huo huo Wizara ya Habari ya Nigeria imedai kuwa, hali ya kiongozi wa nchi hiyo ni nzuri.
Wanigeria wakimtaka Buhari ajiuzulu
Tangu alipoondoka nchini Nigeria miezi mitatu iliyopita na kwenda
Uingereza kwa matibabu, Rais Muhammadu Buhari hajawahi kufanya mahojiano
na vyombo vya habari au kuonekana hadharani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.