Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria kwa mara
nyingine amemtaka mkoloni mkongwe wa Ulaya yaan Ufaransa aiombe radhi
rasmi nchi yake kutokana na jinai kubwa alizowafanyia wananchi wa
Algeria.
Rais huyo wa Algeria alisema hayo
jana wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa nchi yake na
kusisitiza kuwa, wananchi wa Algeria wanamtaka mkoloni wa jana yaani
Ufaransa kuwaomba radhi rasmi kutokana na ukatili, jinai, mateso na
masaibu mengi aliyowasababishia.
Kabla ya hapo pia Algeria ilikuwa
imeitaka Ufaransa iwaombe radhi wananchi wa Algeria kutokana na ukatili
na jinai alizowafanyia kwenye kipindi cha miaka 132 ya ukoloni wake
katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria. |
Hii ni katika hali ambayo rais mpya wa
Ufaransa, Emanuel Macron aliitembelea Algeria mwezi Februari mwaka huu,
wakati alipokuwa anagombea urais wa Ufaransa na kukiri katika ziara hiyo
kwamba ukoloni wa nchi yake huko Algeria uliofanyika katika miaka ya
kuanzia 1830 hadi 1962 ilikuwa ni jinai dhidi ya binadamu.
Zaidi ya watu milioni moja wa Algeria
waliuliwa na wakoloni makatili wa Ulaya yaani Ufaransa katika vita vya
ukombozi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Tangu wakati huo hadi hivi sasa,
wananchi wa Algeria wamebakiwa na makovu ya jinai na ukatili
waliofanyiwa na Wazungu hao wa Ulaya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.