Watu 12 wameripotiwa kuuawa katika mapigano
ya hivi karibuni kabisa baina ya waasi na jeshi la Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa wenye machafuko wa Kivu Kusini,
mashariki mwa nchi hiyo kubwa na pana ya katikati mwa Afrika.
Shirika la habari la AFP
limemnukuu msemaji wa jeshi la Kongo katika jimbo la Kivu Kusini,
Kepteni Dieudonne Kasereka akisema kuwa, mapigano hayo yametokea baina
ya waasi wa Mai Mai na askari wa serikali na kupelekea kuuawa wanajeshi
wawili na waasi tisa pamoja na raia mmoja.
Kepteni Kasereka ameongeza kuwa, kuna
uwezekano wa kuongezeka idadi ya wahanga wa mapigano hayo ambayo
yametokea katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa Mai Mai. Wanachama
wanne wa waasi hao wametiwa mbaroni na jeshi la serikali ambalo
limefanikiwa pia kupata silaha nzito kutoka katika eneo hilo lililokuwa
linadhibitiwa na waasi.
Waasi wawili wa Mai Mai wakiwa nje ya kibanda katika kijiji cha Kalenge, mashariki mwa DRC. |
Mapigano makali yamezuka tangu siku chache zilizopita baina ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa Mai Mai, mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa zinasema kuwa kuna makundi
kadhaa ya waasi wa kabila la Mai Mai katika mikoa ya Kivu Kaskazini na
Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Maafisa wa jeshi la nchi hiyo aidha
wamekiri kuwa, waasi wa Mai Mai wamefanikiwa kuteka sehemu nne za eneo
la Fizi zilizokuwemo mikononi mwa jeshi la serikali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.