Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.
Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Msondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi mauti yanamkuta.
BLOG inatoa mkono wa rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa Shaaban Dede kwa kuondokewa na mkongwe huyu wa muziki.
Mola aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi - AMIN
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.