Leo July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.
Prof. Lipumba alitangaza kuwafuta uanachama Wabunge wanane na Madiwani wawili kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kinidhamu, kukihujumu chama, Kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo hawana sifa za kuendelea na Ubunge
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.