NA ZEPHANIA MANDIA TAREHE 26/07/2017
Kampeni ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kumtua mwanamke ndoo kichwani, imeanza kufanikiwa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza Shanif Mansoor, kuwakabidhi Wananchi wa jimbo lake jumla ya visima 11 na kuvifanyika ukarabati visima 13.
Kabla ya visima hivyo kukabidhiwa, baadhi ya wakazi hao walikuwa wakikabiliwa na adha ya kubwa ya ukosefu wa Maji safi na salama, lakini baada ya visima hivyo kukabidhiwa sasa ni chereko ndani ya vinywa vyao, huku wakieleza pia ubovu wa visima walivyojengewa zamani.
Baada ya hatua hiyo safari ya Mbunge huyo ikaelekea katika kata ya Hungumarwa, ambapo amekabidhi mifuko 22 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Nyanhiga, Nela Sekondari pamoja na ujenzi wa Zahanati.
Hadi ziara hiyo
inakamilika zaidi ya shilingi million ishirini zimetumika kutatua changamoto
mbalimbali, zinazoikabili sekta ya elimu wilayani Kwimba, afya, miundombinu
pamoja na sekta ya Maji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.