Mkuu wa Takukuru Mwanza Ernest Makale. |
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF unaoshuhudia kupita katika kipindi kigumu kwa baadhi ya wajumbe wake na wagombea kuburuzwa mahakamani kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya utakatishaji fedha, hatimaye leo Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini, TAKUKURU mkoa wa Mwanza imethibitisha kuwashikilia watu 10 wanafamilia wa soka wanaoshukiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Mkuu wa Takukuru Mwanza Ernest Makale amethibitisha kuwa watu hao kushikiliwa tokea jana saa 3 usiku na wameachiwa leo mchana kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na watakapojiridhisha juu ya tuhuma zinazowakabili hatua zitachukuliwa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Makale aliwataja watuhumiwa hao ni pamoja na Msimamizi mkuu wa Ndondo Cup ambaye pia ni mgombea Shaffih Dauda, Almas Kasongo, Elias Mwanjali, Leonard Malongo ambaye ni mpiga kura na katibu chama cha soka Mwanza (MZFA), Osuli Charles Osuli huyu ni mpiga kura toka mkoa wa Simiyu, na Benard Lugola kutoka mkoani Shinyanga.
Wengine walionasa kwenye mtego huo ni Richard Kiyenze mpiga kura kutoka Tabora, Kelvin Patrick Chella naye ni mpiga kura, Razack Juma Ilunga mpiga kura kutoka Tabora na Ephrahim Majinge ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF ambaye pia ni mgombea.
Watuhumiwa hao walio kwenye sekeseke hilo wanashukiwa kuwa, walikuwa katika mikakati ya kutafuta kura kwa njia chafu ya rushwa na kuendesha kampeni kabla ya wakati.
Taarifa zaidi inasema kuwa wanafamilia hao walitumia mgongo wa Ndondo Cup kufanya jambo lao usiku wa saa 3 jana na ndipo walipotiliwa shaka na kufuatiliwa na kutiwa mikononi mwa Takukuru ambao wamethibitisha kuwashikilia tokea jana usiku na kuwaachia kwa dhamana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.