Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka Tanzania wakati mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA.
Mkuu
wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa
washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia
simu za mkononi yanayodhaminiwa
na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya
simu za mkononi ulimwenguni GSMA
Airtel na GSMA wandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi
Kampuni ya
simu za mkoni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa
mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi
ambayo yanafanyika
jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.
Mashindano
hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na
muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA yanajumuisha
washiriki
kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka Ghana, Kenya, Uganda
na Tanzania watachuana kutengeza suluhu kwenye maeneo makuu matatu,
yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya jumla
(bulk payment )na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva
na Airtel yaani ( Airtel Comviva mobile wallet). Tanzania imepata
fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama kiongozi
katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga mifumo ya
malipo ya simu ( mobile money payment) Hivyo ni fursa
ya kipekee kwa wajisiriamali wa kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za
mifumo ya malipo ya simu za mkononi zitakazotumika barani Africa.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel
Tanzania Isack Nchunda alisema ushirikiano huu ni muhimu kwa vile
unawezesha wajasiriamali
wa TEKNOHAMA kuja na suluhu ambayo itaweza kusaidia kufanya malipo
kupitia simu za mkononi kwa haraka na hivyo kuokoa kupoteza muda kupanga
foleni kusubiria kufanya malipo.
Sisi
Airtel Tanzania tumekuwa msitari wa mbele kuwezesha wajasiriamali kwa
njia mbali mbali. Kwa kupitia mashindano tunaendeleza uwezeshaji huo
kwani kwa kila suluhu
itakayopatikana haitaishia hapa mbali itaendelea kuboresha na kuwekwa
kwenye mfumo wa malipo ya simu za mkononi, alisema Nchunda.
Kwa
upande wake, Mkuu wa kitengo cha Teknohama GSMA Gareth Pateman alisema
washiriki wa mashindano hayo wanaweza kutengeneza suluhi moja au mbili
katika zile tatu
huku mshindi akipata ticketi ya kwenda Barcelona, Spain huku akiwa
amelipiwa gharama zote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.