KWAMBA TAREHE
06.07.2017 MAJIRA YA SAA 12:30HRS KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA
KIJIJI CHA MISUNGWI KATA NA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI
AMBAO NI DEREVA NA KONDAKTA WA GARI LENYE NAMBA T.574 AZU AINA YA SCANIA BUS
MALI YA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS , WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.SUDI YUSUPH
MIAKA 35, DEREVA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS, MKAZI WA BUZURUGA –MWANZA
NA 2.BONIPHACE MASHAURI, MIAKA 52, KONDAKTA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS,
MKAZI WA MUSOMA – MARA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA
KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA “MIRUNGI” KIASI CHA MABUNDA 112, KITENDO
AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI POLISI WALIPATA
TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA BUS TAJWA HAPO JUU LINALOFANYA SHUGHULI YA
KUSAFIRISHA ABIRIA KUTOKA MUSOMA KWENDA DODOMA LINAJIHUSISHA PIA NA KUSAFIRISHA
MADAWA YA KULEVYA (“MIRUNGI”). AIDHA BAADA YA ASKARI KUPATA TAARIFA HIZO
WALIWEKA MTEGO, NDIPO JANA TAREHE TAJWA HAPO JUU BUS HILO LIKIWA LINATOKEA
MUSOMA KWENDA DODOMA LILIPOFIKA KIJIJI CHA MISUNGWI ASKARI WALILISIMAMISHA KISHA LIKAFANYIWA UPEKUZI NA KUKUTWA LIKIWA LIMEBEBA MIRUNGI AMBAYO NI KUNDI LA MADAWA YA KULEVYA KIASI CHA BUNDA 112, YALIYOKUWA
YAMEHIFADHIWA NDANI YA MABEGI KISHA KUWEKWA NDANI YA BUTI YA GARI.
MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE
NI UTINGO WA GARI HILO AMETOROKA, JUHUDI ZA KUMTAFUTA BADO ZINAENDELEA. POLISI
WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
WATUHUMIWA WOTE WAWILI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UCHUNGUZI NA MSAKO WA
KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA
UTUMIAJI, UUZAJI NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KATIKA MKOA WA MWANZA
BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI
AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI WAMILIKI WA
MABASI KUACHA KABISA TABIA YA KUJIHUSISHA NA USARISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA
KWANI NI KOSA LA JINAI NA ENDAPO GARI LITAKAMATWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHULIWA DHIDI YA
MWENYE MALI. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA
WAHALIFU NA UHALIFU MAPEMA ILI WATUHUMIWA WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE
VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M)
MWANZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.