Katika kesi namba 218 ya 2017, Kupitia Nasorro katuga Wakili wa Jamhuri, Halima Amesomewa shitaka la kutumia lugha ya matusi Dhidi ya Rais Magufuli "Rais anaongea Hovyo, Afungwe Breki" Hata hivyo alipoulizwa kama nikweli Mdee alikana shitaka hilo.
Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee alifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Leo Jijini Dar es salaam majira ya Asubuhi.
Halima Mdee (Chadema), alikamatwa Julai 4 Jioni, na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi. Kwa kile kilichodaiwa alitoa lugha ya kumtukana Rais Magufuli.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.