Tume ya Mishahara na Marupurupu ya Watumishi
wa Umma nchini Kenya imetangaza kupunguzwa kwa mishahara ya maafisa
wakuu wa serikali wakiwemo rais, mawaziri na magavana.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bi Sarah
Serem ametoa mpangilio mpya wa malipo ambao anasema utaokoa jumla ya Sh8
bilioni (dola milioni 80 za Marekani) kila mwaka na kupunguza jumla ya
mishahara inayolipwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.
Kwa mujibu wa tangazo la Tume ya
Mishahara na Marupurupu ya Watumishi wa Umma nchini Kenya sasa Rais wa
nchi atakuwa akilipwa Sh1.4 milioni (sawa na dola 14,000) kila mwezi,
badala ya Sh1.65 milioni (dola 16,500), huku naibu wake akipokea Sh1.2
milioni (dola 12,000).
Aidha taarifa hiyo ya Tume ya SRC
imeeleza kuwa, mawaziri watakuwa wakilipwa Sh924,000 (dola 9,200), Spika
wa Bunge Sh1.1 milioni (dola 11,000) nao magavana wa kaunti Sh924,000
(dola 9,240). Mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa tarehe 8 Agosti,
2017.
Rais Uhuru Kenyattaf na naibu wake William Ruto.
Tume hiyo imependekeza kufutiliwa mbali kwa marupurupu ya kipimo cha
usafiri wa magari kwa magavana na wabunge na badala yake hilo litakuwa
likifidiwa na mfumo mpya wa marupurupu kwa kuzingatia kanda. Bi Sarah
Serem amesema kuwa, maafisa wa serikali walikuwa wakitumia vibaya mfumo
wa marupurupu wa kupimiwa usafiri wa magari.
Magavana na manaibu wa magavana pia
hawatakuwa wakilipwa tena marupurupu. Wabunge, ambao wamekuwa wakilipwa
marupurupu kwa kuhudhuria vikao vya kamati mbalimbali, pia watakosa
marupurupu hayo. Viongozi wa serikali ya upinzani bungeni, ambao pia
walikuwa wakipokea marupurupu ya majukumu maalum pia hawatalipwa tena
marupurupu hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.