ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 20, 2017

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSAFIRSHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI KIASI CHA KILO 31, WILAYANI NYAMAGANA.

 
KWAMBA TAREHE 19.02.2017 MAJIRA YA SAA 7:25HRS ASUBUHI KATIKA STANDI YA KAMANGA FERI KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA STANSLAUS LUCAS, MIAKA 38 MKURYA NA MKAZI WA NYAKATO NATIONAL, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI KIASI CHA KILO 31, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIFIKA  HAPO KWENYE STANDI YA KAMANGA FERI MAJIRA TAJWA HAPO JUU AKIWA NA GARI LENYE NAMBA T.701 AINA YA NOAH, KISHA ALITOA BOKSI MOJA KUTOKA NDANI YA GARI LAKE NA KUWAKABIDHI MAWAKALA WA MAGARI YAENDAYO KIGOMA NA KUWAELEZA KUWA MZIGO WAKE ANAOMBA USHUSHWE KIBONDO. MAWAKALA WA MAGARI WALIPATA MASHAKA JUU YA HILO BOKSI NDIPO WALIMWOMBA MTUHUMIWA AWAELEZE KITU ALICHOKIWEKA NDANI YA BOKSI, LAKINI MTUHUMIWA HAKUWEZA KUELEZA KITU CHOCHOTE, NDIPO WALILIFUNGUA NA KULICHEKI  NDANI NA KUONA LIKIWA LIMEJAA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI.

AIDHA BAADA BOKSI KUONEKANA LIKIWA LIMEWEKWA  MIRUNGI, MAWAKALA WA MAAGARI WALIMSHIKILIA MTUHUMIWA KISHA WAKATOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMTIA NGUVUNI MTUHUMIWA PAMOJA NA KULIIFANYIA UPEKUZI GARI LAKE AMBAPO LILIKAMATWA BOKSI LINGINE LIKIWA NA MIRUNGI, AIDHA MABOKSI YOTE MAWILI YALIYOKAMATWA YALIKUWA NA MIRUNGI  KIASI CHA KILO 31.


KATIKA MAHOJIANO YA AWALI ALIYOFANYIWA MTUHUMIWA NA POLISI ALIKIRI KUWA NI KWELI AMEKUWA AKIJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA YA AINA YA MIRUNGI KWA MUDA MREFU, ALIDAI KUWA MIRUNGI AMEKUWA  AKIITOLEA SIRARI NA KUISAMBAZA SEHEMU MBALIMBALI YA JIJI LA MWANZA NA MAENEO YA JIRANI, LAKINI ALIDAI KUWA MIRUNGI HIYO ALIYOKAMATWA NAYO ALIKUWA AKITAKA KUISAFIRISHA KWENDA  KIBONDO MKOANI KIGOMA. POLISI WANAENDELEA NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA ILI KUWEZA KUBAINI MTANDAO WA WATU WENGINE ANAOSHIRIKIANA NAO KATIKA BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWAPONGEZA MAWAKALA WA MAGARI WOTE WA STANDI YA KAMANGA FERI KWA USHIRIKIANO MZURI WA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA AMBAO WAMEUONESHA KWA WANANCHI, HIVYO ANAWASIHI WATU WOTE WA JIJI LA MWANZA WAIGE MFANO WA AINA KAMA HII. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI JUU YA WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA, UTUMIAJI NA USAFIRISHAJI WA MADAWA HARAMU YA KULEVYA, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO SHERIA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.