Wanufaika wa Programu ya WanaNzengo Airtel Fursa awamu ya pili katika Picha ya Pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo ya ujasiriamali na kupokea fedha kwa njia ya Airtel Money. |
Wananchi wa Nzega Mjini wazidi kunufaika na fedha za programu ya WanaNzengo Airtel FURSA
Baada ya mafanikio makubwa ya Programu ya WanaNzengo Airtel FURSA uliozinduliwa Oktoba mwaka jana, na jumla ya shilingi milioni 20 kutolewa kama mikopo isiyokuwa na masharti magumu kwa vikundi 20 vya wajasiriliamali takribani 100 wa mji wa Nzega, tayari vikundi vingine 10 vyenye jumla ya watu 50 vimenufaika na fedha kiasi cha shilingi million 10 ambazo zimetolewa katika awamu ya pili.
Akizungumzia mafanikio hayo mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe alisema “Tangu tuzindue program hii miezi miwili iliyopita tayari program hii imeendelea kuwa kivutio kikubwa cha uwezeshaji miongoni mwa wananchi wa kada mbalimbali ndani ya jimbo la Nzega mjini. Program hii imekuwa kuvutio kwa wafanyabiashara, wajasiriamali pamoja an wafanyakazi mbalimbali. Tunapongeza kwa dhati jitihada za pamoja baina ya Airtel Tanzania na Nzega Urban Trust Fund ambayo ni taasisi niliyoanzisha ili kuinua hali ya maisha ya wananchi wenzangu hapa Nzega Mjini.”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Nzega Urban Trust Fund, Bw. Felician Andrew alisema kuwa “Tunaishukuru sana Airtel Tanzania kupitia mpango wao wa Airtel FURSA kwani umeweza kuwafikia hadi watu wa kada ya chini kabisa hapa Nzega, mara ya kwanza wakati tunaanza programu hii tulitoa milioni 20 na sasa fedha zote zimeanza kurejeshwa na tumekusanya milioni 10 kwa njia ya Airte Money fedha ambazo ndizo tumezitumia tena kuzirudisha kwa wanafaika wapya kabisa kwa kutumia mfumo ule ule wa Airtel Money”
Naye Bi. Debora Mhamba mmoja wa wanufaika kutoka kikundi cha Ebenezer alisema kuwa “mpango wetu ni kuwa kikundi chenye uwezo mkubwa wa kusimamia fedha zake na kupanua biashara zetu katika maeneo mengi zaidi nje ya Nzega, hivyo tutatumia vyema fedha hizi ili kufikia malengo yetu na kurudisha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kunufaika na fedha hizi”
Kwa upande wake Meneja huduma za kijamii, Hawa Bayumi alisema tunafurahi kuona mradi unaendelea vyema na vikundi vingi vinaendelea kufikiwa zaidi, lengo letu ni kufika wasiriamali wengi zaidi ifikapo mwisho wa mwaka. Natoa wito kwa wakazi wa Nzega mjini kuendelee kuitumia fursa hii vyema ili kuimarisha mitaji na biashara zetu na hivyo kuleta chachu katika maendeleo ya jamii zetu na nchi kwa ujumla”
Makabidhiano haya ya fedha hizi yalifanyika katika Ofisi ya Nzega Urban Trust Fund hapaNzega Mjini na kushuhudiwa na kuhudhuriwa na Meneja wa Airtel Mji wa Nzega, Bw. Abraham Mvella pamoja na maofisa mbalimbali wa Ofisi ya Mbunge.
Zoezi hili la utoaji wa pesa lilifanyika baada ya kumaliza uhakiki wa vikundi zaidi ya 100 vilivyotuma maombi na kufanyiwa uhakiki na tathimini ya biashara zao ambapo vikundi kumi vikaibuka kidedea kuwa na sifa zaidi ya vikundi vingine kuweza kunufaika na fedha za Programu hii.
Utoaji wa fedha za mikopo kwa awamu ya pili uliambatana na mafunzo ya jinsi ya kufanya marejesho ya fedha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.