Msimamizi mkuu wa kituo cha ORICA Mkoani Geita,Yahya Ruyaga akimkabidhi Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha nyakumbu ,Abdallah Amiry Kiroboto . |
Msimamizi mkuu wa kituo cha ORICA Mkoani Geita,Yahya Ruyaga,akielezea zumuni la kutoa msaada. |
Yahya Ruyaga akikabidhi shuka 30 ambazo wamezitoa kwenye kituo cha afya cha nyakumbu. |
Yahya Ruyaga akikabidhin risti ya manunuzi ya vifaa hivyo kwa mganga mfawidhi wa kituo hicho. |
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha nyakumbu ,Abdallah Amiry Kiroboto akishukuru baada ya kupokea msaada huo. |
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha nyakumbu ,Abdallah Amiry Kiroboto akizungumzia msaada huo ambavyo utaweza kurahisisha kazi zao. |
Msimamizi msaidizi wa Kampuni ya ORICA Mwandisi Paschal Malugu akielezea dhumuni la kutoa misaada hiyo. |
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa. |
Wafanyakazi wa kampuni ya ORICA pamoja na watumishi wa kituo cha afya cha nyakumbu wakiwa katika picha ya pamoja. |
Wafanyakazi wa kampuni ya ORICA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi la kukabidhi vifaa tiba. PICHA NA JOEL MADUKA
Kampuni ya ORICA ambayo inafanya kazi za kulipua miamba ya dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) na Buzwagi Imetoa vifaa tiba kwenye kituo cha afya cha Nyakumbu kilichopo kwenye kata hiyo wilaya na Mkoa wa Geita vyenye thamani ya shilingi Milion mbili(2000,000)
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ,Msimamizi msaidizi wa kituo cha Orica mwandisi Pascal Malugu,amesema kuwa walifikiria kuwa sio vyema kwenye jamii ambayo wanafanyia kazi kutokutoa mchango wowote ambao utasaidia jamii hivyo wakaguswa na kuamua kutoa vifaa tiba ambavyo vitasaidia kutoa huduma za kiafya huku akitoa wito kwa makapuni mengine kujitolea misaada mbali mbali.
“Leo hii si mara ya kwanza katika jamii kutoa misaada kwani tulishawahi kutoa kifaa kingine cha Eqbet kwenye hospitali ya Geita na sisi tuliona sio vyema kutotoa misaada ambayo itasaidia jamii inayotuzunguka lakini niombe Mashirika na Makapuni mengine kuguswa na kutoa misaada kwani hii ndio dini safi kuwasaidia ambao ni wagonjwa”Alisema Malugu.
Hata hivyo kwa upande wake msimamizi mkuu wa kampuni hiyo,Yahaya Ruyaga ameelezea kuwa wanaamini kuwa msaada ambao wameutoa utapunguza adha iliyokuwepo kwenye kituo hicho na kwamba ni mwanzo tu kwani wanajipanga kuendelea kutoa mchango zaidi kwenye maeneo yaliyopo ndani ya Mkoa wa Geita.
“Sisi kama saiti ya Geita tulikaa wafanyakazi na kuweza kufikiria kwamba je sisi kama sisi tunaweza kufanya kitu gani kwenye jamii ili walau na sisi tuweze kuleta faida kwenye jamii inayotuzunguka ndipo tulipoamua kuunda tume ya kufuatilia vituo vyetu vya afya vilivyopo kwenye halmashauri ya mji mwisho wa siku tukajua kituo cha Nyakumbu kina uhitaji mkubwa ndipo tulipoamua kutoa msaada huu wa vifaa tiba”Alisema Ruyaga.
Aidha mganga mfawidhi wa kituo hicho,Abdallah Amiry Kiroboto amesema kuwa vifaa walivyopatiwa vitawasaidia kurahisisha kazi na kwamba kwa sasa wataweza kupima magonjwa ya kisukari kutokana na kupatiwa kifaa hicho huku akiomba msaada kwa wadau wengine kufika katika kituo hicho na kuwasaidia kwani wana upungufu mkubwa wa vifaa vingi vya kufanyia kazi.
Baadhi ya wananchi ambao walikuwepo kwenye makabidhiano hayo wameishukuru kampuni hiyo kwa moyo wa kujitolea huku wakiomba makampuni ambayo yamo ndani ya mgodi wa GGM kuiga mfano wa kampuni hiyo.
IMEANDALIWA NA www.madukaonline.Blogspot.com
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.