WAZIRI wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo,amemwagiza Kamishina wa madini kanda ya ziwa kutembelea migodi yote na kuikagua ili kujua hali ilivyo na kuakikisha wanatoa mashariti katika migodi yote mikubwa,ya kati na midogo.
Hayo ameyasema wakati alipowatembelea wachimbaji kumi na tano ambao walifukiwa na kifusi kwenye mgodi wa RZ union uliopo kwenye kijiji cha mawemeru Kata ya Nyarugusu wilaya na Mkoa wa Geita.
Prof,Muhongo amemwagiza kamishina wa madini kuakikisha anafanya ukaguzi na kutembelea migodi yote na kwamba kufikia tarehe 16 ya mwezi wa tatu awe ametoa taarifa ya hali ilivyo kwenye migodi ambayo hatakuwa ametembelea.
“Kamishina nimekwisha waelekeza tembeleeni Migodi yote mkague na kwasababu watu wanaendelea kuchimba kama nyie ni wachache tuongezeni nguvu kutoka wizarani,kutoka stamiko,siorojiko au chuo kikuu leo ni tarehe 17 hadi kufikia 16 mwezi ujao nipewe ripoti ya ukaguzi”Alisisitiza Prof Muhongo.
Kamishina Msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria magharibi Yahaya Samamba ,amemweleza waziri wa nishati na madini sababu zilizopelekea kuanguka ni kutokana na kuzidiwa kwa udongo uliokuwa juu pamoja na kuwa ni mgodi wa muda mrefu hivyo timba zilikuwa zimekwisha anza kuoza na kwamba hatua ambazo zimechukuliwa hadi sasa ni mgodi kufungwa hadi yale maelekezo waliyopatiwa yatakapo kuwa yamekamilika.
“Uchunguzi uliofanyika umeonyesha kuwa mgodi huu umeanguka kutokana na kuzidiwa na udongo laini juu pia mwamba laini ulioza kiasi cha takribani mita 15 kutoka usawa wa ardhi lakini pia sambamba na hilo mgodi huu una muda mrefu zaidi ya miaka mitatu kwa hiyo zile sapoti kwa maana ya timba zilikuwa zimekwisha hanza kuoza na tulikuwa tumekwisha wapo maelekezo wakati wakiwa kwenye marekebisho ya kuweka chuma ndio ajali hii iliweza kutokea kazi inayoendelea hivi sasa ni kutoa maji kwenye shimo ili kuakikisha mazingira yanakuwa mazuri ili kufanya yale ambayo yameagizwa na kamishina wa madini”Alisema Samamba.
Kwa upande wake msemaji wa mgodi huo na mwanasheria,Francis Kiganga ,amemwomba Waziri wa nishati na madini kutia sahini ya hati ya uhamishaji miliki kwa maana pande zote mbili wamekubaliana kwa muuzaji abaki na asilimia 15 na mnunuzi ahamishiwe asilimia 85.
Hata hivyo ombi hilo alikukubaliwa na waziri wa nishati na madini hadi pale mgodi huo utakapokuwa umetimiza mashariti ambayo wamepatiwa.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi,amemweleza waziri Muhongo kuwa wamefatilia kuakikisha vijana wanapatiwa mikataba ya kudumu .
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wenzake ambao walinusurika kwenye ajali hiyo Ansenti Masanja amemshukuru waziri Muhongo kwa kuwatembelea na kuja kuwajulia hali zao ikiwa ni pamoja na kuwapa pole.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.