ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 17, 2017

PAPA FRANCIS: TAMAA YA MADOLA MAKUBWA IMESABABISHA UMWAGAJI DAMU DUNIANI.


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametahadharisha kuhusiana na hatua za kupenda vita za madola makubwa duniani na kusema kuwa, tamaa ya madola hayo imesababisha umwagaji duniani.
Papa Francis amesema kuwa, madola makubwa yakiwa na lengo la kunufaika na kushika hatamu za uongozi yamekuwa sababu ya kutokea vita na umwagaji damu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema bayana kwamba, yanachokitafuta madola makubwa duniani ni nguvu, satwa na kunufaika. Papa Francis ameeleza kuwa, siasa za kupenda vita zimekuwa ni tishio kubwa mno kwa maisha na utulivu wa walimwengu.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa wito wa kudumishwa amani na kuchukuliwa hatua za kukomesha vita na machafuko katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani anabainisha hayo katika hali ambayo, maelfu ya watu wamepoteza maisha yao katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni natija ya uingiliaji wa kijeshi wa Marekani na waitifaki wake wa Kimagharibi katika nchi za Iraq, Syria na Yemen.
Aidha asasi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la Umoja huo zinakosolewa mno na walimwenghu kutokana na kuathiriwa katika utendaji wake na madola makubwa.
Udhaifu wa taasisi hizo umezifanya zshindwe kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kubakia kama wenzo unaotumiwa na madola makubwa kwa ajili ya kufikia malengo yao.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.