Rais wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band Fabrice Kinyenya (kulialia) Akiwa anaimba katika usiku wa kuwatambulisha bendi hiyo wakazi wa jiji la Arusha < /div>
wanamusiki wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa wanaonyesha kiwango chao ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha</ span>
waimbaji wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa fanya yao
Wanenguaji wa bendi ya Mount meru Rickernest Music Band wakifanya yao
Rais wa bendi akifanya mambo ndani ya ukumbi wa Triple A < /div>
wakwanza kulia ni mmoja wa wakurugenzi wa bendi ya Mount meru Rickernest Music Band Akifatilia onyesho ,wa pili kushoto ni mkurugenzi mwingine wa bendi hiyo Prisca Aloyce wote wakiwa wanafatilia kwa makini onyesho.
Habari picha na Woinde
Shizza,Arusha
Bendi mpya ya
mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mount Meru Ricknest music bandi
imezinduliwa rasmi mkoani Arusha huku ikiwaaidi huku ikiwaaidi wapenda mziki wa dance burudani
isiokuwa na mpinzani
Akiongea na waandishi wa habari jana mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo Ernest mlolere alisema kuwa kwa sasa wameitambulisha bendi hiyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha tu na wanataajia kuzindua bendi hiyo rasmi katika siku yawapendanao (valentine day ) hapa hapa jijini Arusha
Alibainisha kuwa bendi hiyo ipo chini ya wakurugenzi watatu akiwemo yeye mwenyewe Erinest Mlolere ,Denis Kaiza pamoja na Prisca Aloyce ambapo wamekaa chini na wakaamua kuanzisha bendi hiyoili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha ,ambao wamekuwa wakikosa burudani ya bendi ya uhakika kwa kipindi cha mda mrefu
Alisema kuwa kumekuwa
na bendi jijini hapa lakini zimekuwa
hazikoshi nyoyo za wapenzi wao wa musiki wa dance hivyo wameona wawaletee
wanamusiki wenye uzoefu ,wenye vipaji vya kutosha ili wananchi wa mkoa wa
Arusha pamoja na jirani kuweza kupata
burudani
Aidha aliongeza
kuwa bendi hii atakaa Arusha tu bali
itakuwa inatembea mikoa mbalimbali ili kuweza kuwapa burudani wapenzi wa music
wa dance wan chi nzima .
“tumejipanga
vyema tunaweza na tunauhakika ujio huu
wa bendi hii utawafurahisha na kuwashika wapenzi wengi wa music wa dance ,kwani
wanamusic ambao wapo katika bendi hii ni wazuri na wanavipaji vya kutosha
nathani unajua kabisa ukiwa na kitu kizuri lazima watu wakipendi naamini kabisa
wanamziki wetu wapenzi wa bendi watawapenda .
Alibainisha kuwa
katika bendi hii pia kuna wana music kutoka katika bendi maarufu za nje ambapo
alitaja baadhi ya wanamusic waliotoka
katika bendi za nje kuwa ni pamoja na rais wa bendi Fabrice Kinyenya (kulialia)
ambapo yeye ametoka katika bendi ya Ferre Gola
pamoja na Katoto (Tanesco) ambaye yeye ametoka katika bendi ya Fally Ipupa wote .
Aliongeza kuwa
wanajua kabisa kuna bendi zilizotangulia
hapa nchini na zinaaminika ila kwa jinsi walivyojipanga yeye na
wanamusic wake anaimani kabisa watazipita bendi zote zilizopo hapa nchini na hata
zile zilianzishwa hivi karibuni zilizopo jijini hapa.
“sasa ivi tupo katika harakati za kupanga siku
ya uzinduzi rasmi wa bendi hii ila hii
leo tumekuja kuwaonyesha wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa kunabendi inayopiga
vizuri sana iliopo hapa mkoani kwao ,na
kwakuwa ni nyumbani tumejipanga kila siku ya jumamosi kuwapa burudani ambapo
tutakuwa tunapiga katika ukumbi wa triple A
Alisema Mlolere
Kwa upande wake Rais wa bendi hiyo Fabrice Kinyenya (kulialia) alipoongea
na waandishi wa habari alisema kuwa
wamejipanga vilivyo kuwapa wapenzi wa musiki wa dance burudani ya uhakika ambayo itamkosha kila mtu nyoyo.
“mimi sipendi kuongea
sana napenda kufanya vitendo zaidi ,wasanii wangu wapo vizuri nanachosema tu ni
wapenzi wa musiki wa dance wasubiri kupata burudani ya nguvu yenye viwango vya
kimataifa ,hapa ni kazi tu hakuna maneno mengi “alisema Fabrice
Alisema kuwa hadi sasa wameshatunga nyimbo za bendi na
watazitambulisha siku ambayo bendi inatambulishwa rasmi ,huku akibainisha kuwa
bendi hiyo inanyimbo nzuri ambazo zitamfurahisha kila mtu
Hii ni bendi ya tatu kuzinduliwa ndani ya jiji la arusha kwan kabla ya hii kipindi cha mwaka uliopita 2016 bendi mbili zilianzishwa jijini hapa ambapo bendi ya kwanza ya mjengoni music band ilizinduliwa na pia kuna bendi ya East Afrika music bandi zote zikiwa ni bendi za musiki wa dance hivyo wakazi wa jiji hili wamenufaika kwa kuletewa music karibu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo wakazi wa jiji hili walikuwa wakipata tabu sana kupata burudani ya muziki wa live bandi .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.