Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema, kwa kuingia Donald Trump katika Ikulu ya Marekani, White House nidhamu ya dunia ya karne ya 20 "imemalizika moja kwa moja" na hali ya mchafukoge ndiyo inayofuatia.
Frank-Walter Steinmeier ameyaeleza hayo katika makala iliyochapishwa na jarida la Kijerumani la Bild na kubainisha kuwa: "Kama ilivyo kila mara, wakati nguvu za madaraka zinapobadilishwa, shaka, hali ya kusuasua na masuali kadhaa yanajitokeza kuhusu mkondo itakaofuata serikali mpya".
Steinmeier ameongeza kuwa leo hii vitu vingi vimo hatarini; na kwa kufanikiwa Donald Trump kuwa rais, dunia ya karne ya 20 imeshafikia tamati moja kwa moja.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, ambaye hapo kabla alishawahi kumkosoa rais mpya wa Marekani amesema hotuba za Trump zinaeneza hisia za chuki.Donald Trump akiapishwa kuwa Rais mpya wa Marekani. |
Naye Naibu Kansela wa Ujerumani Sigmar Gabriel ametoa matamshi yanayofanana na ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuhusu rais mpya wa Marekani. Gabriel amesema kuhusu hotuba aliyotoa Trump baada ya kutawazwa kuwa rais mpya wa Marekani kwamba: 'lugha ya ukereketwa wa kizalendo' ya rais wa Marekani inakumbusha matamshi ya kisiasa ya wahafidhina na wenye fikra mgando wa muongo wa 1920.
Donald Trump aliapishwa siku ya Ijumaa kuwa rais wa 45 wa Marekani; ambapo katika hotuba yake ya mwanzo kama rais wa Marekani aliwaahidi Wamarekani kuwa katika masuala yote, ataipa kipaumbele cha kwanza Marekani na maslahi ya nchi hiyo…/
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.