MAJAMBAZI WAWILI WAUWAWA JIJINI MWANZA.
NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
WATU wawili wanaosadikika kuwa majambazi Eric Magese (22), na Peter aliyejulikana kwa jina moja, (25-27), wameuawa huku silaha moja ikipatikana Jijini hapa wakati wakijaribu kuwatoroka Askari Polisi walipokuwa wakiwapeleka mahali ambapo wenzao wamejificha ili waweze kufanya uvamizi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mnamo january 20,2016 saa 2 Usiku, katika mtaa wa Kiloleli A Kata ya Nyasaka wilayani Ilemela, Ilipatikana silaha moja aina ya Short Gun yenye namba TZ CAR 103283 ikiwa na risasi tatu ambayo inadaiwa walipora kwenye kampuni ya ulinzi ya Malika Security Servise Limited.
Kwa mujibu wa Kamanda Msangi amesema kuwa Majambazi hao walikuwa wakitafutwa na Polisi baada ya kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo ya kitangiri Disemba 19 mwaka jana, saa 4 usiku walipovamia duka (Super Market iitwayo Stop na Pax) ambapo walimjeruhi kwa risasi mlinzi lakini hawakufanikiwa kupora kitu chochote.
“Majambazi hao pia walifanya unyang’anyi wa kutumia siraha january 2 mwaka jana saa4 Usiku katika mta wa Nyasaka ambapo walivamia duka la bidhaa mbalimbali mali ya Gasper Johas (40) kisha wakapiga risasi moja hewani na kupora fedha Sh.4 milion" amesema Msangi.
Amefafanua kuwa wakati Askari wakiendelea kuwatafuta majambazi hao zilipatikana taarifa kutoka kwa raia wema aikieleza kuwa wameonekana mjini Mwanza, ndipo Askari waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Eric na alipo hojiwa alikiri kuhusika katika matukio tajwa hapo juu kisha aliwapeleka nyumbani kwake ambapo kulipatikana silaha hiyo na kueleza kuwa alikuwa akishirikiana na mwenzake Peter ambaye naye alikamatwa.
Askari waliendelea kuwahoji na ndipo walipoeleza kuwa walipanga kuvamia maduka mengine Jijini hapa maeneo ya Kirumba wakishirikiana na wenzao wawili ambao majina yao yamehifadhiwa na kwamba watu hao walikubali kuwapeleka askari hadi eneo ambalo walipanga kukutana ili wafanye uvamizi.
Amesema kwamba Majambazi hao walipofika na Askari katika eneo hilo walianza kupiga kelele kama ishara ya kuwatorosha wenzao na kuanza kuwakimbia na ndipo walifyatua risasi kadhaa hewani wakiwaamuru wasimame lakini hawakusimama.
Baada ya kuona hivyo Askari walifyatua risasi za mguuni na kwamba kwa bahati mbaa ziliwalenga maeneo ya juu na kisha kufariki dunia wakati wakipelekwa Hospitalini na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi.
Upelelezi na msako bado unaendelea wa kuwakamata majambazi wengine ambao bado hawajapatikana na Kamanda Msangi ametoa wito kwa wananchi wa Jiji na mkoa wa Mwanza kuwaelimisha vijana waache tabia ya kujihusisha na uharifu wa kutumia silaha kwani ni kosa la jinai.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.