ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 15, 2016

U20: KAGERA SUGAR 1 v 1 YANGA, CHRISTOPHER MSHANGA AWASAWAZISHIA BAO DAKIKA ZA MAJERUHI KAGERA KWENYE MCHEZO WA UFUNGUZI LEO KAITABA.


Na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ndie aliyekuwa Mgeni rasmi leo kwenye Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 za klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom iliyoanza kutimua vumbi hii leo Novemba 15, 2016. Mchezo huu wa ufunguzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na kushuhudia Timu wenyeji Kagera Sugar wakiumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Timu ya Yanga.

Kipindi cha kwanza kilimalizika bila ya kufungana, Kipindi cha pili dakika ya 69 Yanga walipata bao la kuongoza kutokana na mpira wa adhabu uliomshinda mlinda mlango wa Timu ya Kagera Samir Mbina Charles. 


Kipindi cha pili dakika za mwishoni Kagera Sugar walisawazisha bao kupitia kwa Christopher Mshanga baada ya beki wa Yanga kukosea na mpira kumtoka na kujikuta akimsindikiza mfungaji huyo kwenye eneo hatari kwenda kushuhudia bao la kusawazisha kwa Kagera huku zikiwa dakika zimeyoyoma.
Vijana wakiwa wamebeba Vibao kuonesha kwa Timu zote kuanza michuano hiyo ya Ligi ya U20 leo kwenye Uwanja wa Kaitaba ambapo Mechi ya Ufunguzi imefanyikia.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ambaye ndie aliyekuwa mgeni rasmi akifunga mkwiji ile kisawasawa kujiandaa kwenda kufunga mkwaju wa penati ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi hiyo ya U20 leo kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu akiupanga kisawasawa mpira 
Shuti ...
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu akifanya yake kwenye ufunguzi wa Ligi ya U-20 .
Kipa aliudaka mpira huo
Timu ya Kagera Sugar U-20 wakiwa tayari kuanza mtanang huo wa Ufunguzi dhidi ya Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam.Timu zote mbili zikiwa tayari kuanza mchezo
Wakisalimiana kabla ya mtanange kuanza
Kagera Sugar U-20
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar U-20










Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar




Msimu wa kwanza wa Timu za U20 umezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Kaitaba na kushuhudiwa na Mashabiki wengi wa soka na mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.
Shadrack Nsajigwa ndie alikuwa akiongoza Timu ya U-20 YangaShadrack Nsajigwa mchezaji wa Zamani na hapa akiitumikia Timu ya U20 ya Yanga.Hakuna kwenda...popote...
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar hii leo wakiwashangilia Vijana wao wa U-20.
katikati ya uwanja patashika lilitokea kipindi cha pili
Mchezaji Yusuph Antony (kulia) wa Yanga akiwakacha wachezaji wa Kagera
Yusuph Suleiman(kulia) akimwendesha mchezaji wa Kagera Sugar
Wazee wa Kazi nao walikuwepo Kaitaba kwenye Ufunguzi...
Kipa wa Timu ya U20 ya Yanga Hamza Abdalah Rwambow akishangilia kipindi cha pili dakika ya 69 baada ya Yanga kupata bao.
Kila mchezaji alikuwa na wake wa kukabaMchezaji Christopher Mshanga (kushoto) akipongezwa baada ya kusawazisha bao dakika za lala salamaShadrack Nsajigwa baada ya Timu ya Kagera kusawazisha bao dakika za majeruhi.
Christopher Mshanga aliyesawazisha bao dakika za lala salama na hapa akihojiwa na Mwandishi wa Habari wa Azam Tv.Mara baada ya mtanange kumalizika walipata picha ya pamoja na Kocha wao msaidizi (kulia) Cretus Mutakyawa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.