Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar es Salaam.
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.
Kwa hatua hiyo Jeshi la Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua bidhaa za feki akiwa pamoja na maafisa wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amezifuma bidhaa hizi feki akiwa pamoja na maafisa wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza.
Sehemu ya shehena za bidhaa za feki zikiwa pamoja. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.