Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016 juu ya matembezi ya hisani ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yanayotarajiwa kufanyika Novemba 19, 2016 Mjini Unguja Visiwani Zanzibar, ambapo Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi ndie anaetarajiwa kuyaongoza matezi hayo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku. |
Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Katika kuhakikisha kuwa vifo vya Watoto Njiti vinapungua hapa nchini,Taasisi ya Doris Mollel Foundation imeandaa Matembezi ya Hisani ili kukabiliana na vifo vya watoto hao kupungua.
Matembezi hayo yenye kauli mbiu ya "Okoa Maisha ya Mtoto Njiti" yatafanyika Visiwani Zanzibar kutokana na Wanawake wengi visiwani humo kukabiliwa kwa asilimia kubwa na suala hilo la Watoto kuzaliwa Njiti.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Doris Mollel amesema kuwa Watoto wengi wanakufa kutokana na kushindwa kupumua wenyewe, hivyo wao kama Taasisi imewasukuma kusaidia suala hilo.
Dorice ametoa shukrani kwa Wadhamini waliojitolea kuasaidia kukabiliana na suala hilo ikiwa ikiwa ni Vodacom Foundation Tanzania, GSM Foundation, Clouds Media Group na UTT AIMS, Michuzi Media Group na wengine wengi.
Pia ametoa shukrani kwa Viongozi wa Serikali kama Mhe. Angela Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wizara za Afya Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mwasiliano, Jacquiline Materu amesema wameamua kudhamini Kampeni hiyo ikiwa ni fursa nzuri kuondoa vifo vya Mama na Mtoto.
Naye Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS amesema wanashirikiana Doris Mollel Foundation toka mwaka Jana amesema watasaidia Kampeni hiyo ya Okoa Mtoto Njiti kuhakikisha wanapunguza vifo vya akina mama na Mtoto.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016, juu ya matembezi ya hiari yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya watoto njiti yanayotarajiwa kufanyika Mjini Unguja, Zanzibar mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku (kulia) akielezea namna walivyoshirikiana na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation katika kufanikisha matembezi hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.