ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 16, 2016

POLISI YAKAMATA NOTI BANDIA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza.

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Yohana Mkalula(42)mkazi wa Maswa Machinjioni anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kosa la kukutwa na noti bandia zenye thamani ya Sh milioni 1.5.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoani hapa Agustino Senga amesema tukio hilo limetokea Novemba 13 saa 11:00jioni ambapo mtuhumiwa alifika katika duka la M-pesa lilipo mtaa wa machinjioni Igoma  mali ya Razalo Eliasi (47) nakutoa noti nne za Sh. 10,000 nakuomba awekewe kwenye simu yake.

Kamanda senga alieleza kuwa kabla ya kupewa huduma hiyo, mwenye duka aligundua kwamba fedha hizo ni bandia nakutoa taarifa Polisi huku mtuhumiwa akiendelea kusubili kupatiwa huduma.

“Polisi walifika eneo la tukio kwa wakati na kuweka mtego dhidi ya mtuhumiwa huyo ndipo walifanikiwa kumtia nguvuni na alifanyiwa upekuzi kwenye mifuko yake ya suruali na kukutwa akiwa na noti nyingine bandia zenye thamani ya shilingi sh.milioni 1.5 ambapo jumla ya pesa zote alizokamatwa nazo ni sh. Milioni 1,540,000/=” alisema Senga

Alieleza kuwa msako wa kuwasaka wenzake aliokuwa akishirikiana nao katika uhalifu huo, bado unaendelea na mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi, pindi uchunguzi utakapo kamilika atafikishwa mahakamani ili hatua za kisheria ziweze kuchukualiwa dhidi yake.

Kamishina Senga ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na mkoa mzima kuendelea kutoa tushirikiano kwa Jeshi la polisi ili liweze kuwakamata na kuumaliza mtandao wa watu wote wanao jihusisha na utengenezaji wa noti bandia huku akiwaasa wananchi kutojihusisha na shughuli za kiuhalifu badala yake wajikite katika kufanya kazi halali za kimaendeleo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.