ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 14, 2016

PICHA ZA ESTER BULAYA YAZODOLEWA.


KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK mdau Boniface Maiga Juma ameandika haya:- 

Kwako Dada yangu Ester Bulaya Salaam sana Amani baada ya salaam, Natumaini u mzima wa afya.
Dhumuni la maandishi haya kwanza ni kukusalimia na hapa naamini Salama zangu umezipata.
Pili ni kuonesha masikitiko yangu kwako na kwa washauri wako ,maana nimeona wakisambaza picha zikionesha ukikagua shughuli za maendeleo zoezi ambalo naamini hufanywa pia na Diwani wa kata husika maana ndio msimamizi wa shughuli za maendeleo ya kata husika,
kitu kilichinisikitisha zaidi ni sanaa uliyoitumia au waliokushauri uitumie, ngoja nikukumbushe kidogo ni hivi karibuni umeonekana hujui tofauti ya mfuko wa jimbo na mfuko wa brauzi,suruali au sketi mpaka kufikia kupata aibu na hatimaye ukasahihisha makosa .
Sasa hilo halijakaa vizuri umekuja na sanaa ya kushika simenti kwa mikono yaani hapa ndio nimesikitishwa maana hata aliye kufungulia mfuko alibaki akikucheka tu maana hata kama ni kuvunja rekodi basi hiyo itakuwa ya hali ya juu,ni hivi karibuni uliandika kuhusu kuimarika kwa afya yako,sasa ukipata magonjwa ya ngozi utamlaum nani ??!
Kitu kingine ni hiyo picha inayomuonesha Diwani wa BUNDA mjini Joash Faith ambaye anaonekana kushika kalai tupu nadhani lengo ilikuwa mtuoneshe manashiriki ujenzi bahati nzuri mmetuachia kumbukumbu ya usanii
Rai yangu kwako na kwa Diwani hata kama ni kutafuta kick jaribuni kujua mazingira mliyomo vinginevyo mnadhalilisha BUNDA na wananchi waliopiga Kura
Naamini salaam zangu zitakufikia
Wasalaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.