ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 14, 2016

ASASI YA EPHC " WADAU WAKIKAA PAMOJA NA KUWA KITU KIMOJA, KUNA TASWIRA YA MABADILIKO ENDELEVU KITUO CHA KULEA WAZEE NA WASIOJIWEZA CHA BUKUMBI MWANZA"

Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali EPHC RURAL Dr. Theophil (kushoto) akikabidhi msaada wa mashuka kwa Afisa Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Afisa mfawidhi wa makao Bi. Jojina Kwesigago katika makabidhiano yaliyofanyika katika kituo cha Kulea wazee na wasio jiweza cha Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
"Sio kwa mtu mmoja mmoja bali inapaswa kukaa pamoja na kuwa kitu kimoja naiona Taswira ya mabadiliko endelevu kituo cha kulea wazee na wasiojiweza cha Bukumbi ZAIDI BOFYA PLAY.


Mkurugenzi wa METDO Bw. Ashraf Omary akikabidhi madawa ya usafi kwa Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza ili avikabidhi kwa Kituo cha Kulea wazee na wasio jiweza kwa kituo cha Serikali cha Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa METDO Bw. Ashraf Omary (kushoto) akikabidhi msaada wa vifaa vya usafi pamoja na mito ya kulalia kwa Afisa Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Afisa mfawidhi wa makao Bi. Jojina Kwesigago, ni misaada kwa kituo cha Kulea wazee na wasio jiweza cha Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza kama sehemu tu ya kuleta mabadiliko katika jamii.
Asasi isiyo ya kiserikali iitwayo EPHC RURAL Tanzania ambayo Mkurugenzi wake ni DR THEOPHIL ikishirikiana Taasisi isiyoyakiserikali iitwayo METDO ambayo Mkurugenzi wake ni ASHRAF OMARY pamoja na MRATIBU WA TAASISI hizi PETER NIBOYE zilizoungana pamoja tukishirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo mwishoni mwa wiki imetembelea Kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza kilichopo eneo la BUKUMBI wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza na Kutoa misaada ya aina mbalimbali.
Moja kati ya misaada iliyotolewa ni pamoja na ungwa wa sembe kwaajili ya chakula, mchele, mavazi, vifaa vya usafi (Mifagio, 6Sabuni, Mopers, Ndoo) , mashuka na mito ya kulalia sanjari na madawa kwaajili ya kituo chao kidogo cha afya.
Dr. Theophil kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya EPHC RURAL akiwasikiliza wazee wa kituo cha Bukumbi Mwanza katika suala zima la mustakbar wa afya zao mmoja mmoja.
Wazee hao pia walipata fursa ya uchunguzi wa Afya bure kutoka kwa madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupatiwa matibabu ya papo kwa hapo kwa wenye uhitaji.

Kuna mengi magumu wanapitia wazee wetu hawa, na ili kuwa kwamua mbinu za dhati zenye utaalamu zahitajika.
Kwa mujibu wa Bw. Ashraf Omary ambaye ni Mkurugenzi wa METDO amesema kuwa tarehe 13/08/2016 imekuwa mwanzo wa shughuli za kusaidia vituo mbalimbali vyenye uhitaji Kanda ya Ziwa, kwani sasa itakuwa ni mwendelezo wa shughuli hizo za utoaji misaada ambapo rasmi mpango wake awamu ya kwanza utahitimishwa tarehe 14 October 2016 katika maadhimisho ya Nyarere Day.

METDO imeahidi kuendelea kusaidia vituo mbalimbali Kanda ya ziwa kikiwemo kituo cha Mitindo Misungwi, Kituo cha wazee Mara, Buhangija Shinyanga, Kituo cha wazee Bukoba na kadhalika.

Wadau walioguswa na zoezi hilo la usafi wa kituo cha Kulea wazee na wasiojiweza wakifagia mazingira ya kituo.
Wadau wa METDO wakifanya usafi ndani ya vyumba vya kambi hiyo ya kulea wazee iliyopo Bukumbi.
Ni usafi usafi kila kona.
Vijana wa Kituo cha Soka cha Marsh Athletics Centre nacho kimejumuika kufanya usafi kwa kituo cha kulea Wazee cha Bukumbi.
Akinadada viongozi, wanahabari wote ni kujumuika hapa.
Familia toka madhehebu ya dini mbalimbali mkoani Mwanza zimehamasika na kujumuika na Asasi ya METDO na hapa akinamama wakishugulika na usafi kudhibiti sehemu korofi ambazo zingehitaji usafi wa kina kama vyoo na bafu.
Bibi huyu asiyeweza kutembea wala hata kujikongoja kutwa akishinda chumbani kwake, ilibidi atolewe nje kupisha usafi uliokuwa ukiendelea vyumbani mwa kambi hiyo ya wazee.







Kazi ni kazi....




Licha ya kuwapatia Dawa ambazo zitawasaidia kwenye mahitaji yao ya kila Siku lakini wadau wameshiriki kumefanya Usafi wa Mazingira,Kudeki Nyumba wanazoishi Wazee hawa, Kufagia Mazingira yote na kufua Nguo za wazee..
Shughuli za usafi zikiendelea huku wazee wengine wakitolewa toka vyumba vyao kupisha usafi kulikuwa na nafasi pia ya kuwasikiliza.
Vijana na watoto kutoka kaya mbalimbali mkoani Mwanza walipozipata taarifa hawakusita kuliunga mkono zoezi la kufanya usafi kituo cha Kulea wazee cha Bukumbi Mwanza.
"Tukio hili tumelifanywa ikiwa ni katika hatua za kuunaunga Mkono Jitihada za Mke wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama JANETH MAGUFULIza kusaidia Wazee wasiojiweza katika Taifa letu kwani sisi kama Jamii ni Wajibu wetu kuhakikisha hawa wazee kwenye hivi vituo wanapata Misaada ya kila hali ambayo itawawezesha kuishi......" alisema Mratibu wa Wana-Habari kutoka Jembe Fm Mansour Jumanne.
Kituo hiki kina jumla ya watu 104, watu wazima ni 83, kwa mchanganuo wa wanawake 56 na wanaume 27, nao watoto ni 21 kwa mchanganuo wa wakike 12 na wakiume 9 wote wakiwa chini ya umri wa miaka 18 hadi miezi 6.
"Sisi sote ni wamoja na tunafanya haya yote tukienzi mema aliyofanya BABA WA TAIFA MWL.NYERERE katika kusaidia Jamii isiyojiweza"
Sehemu ya jumuiko ndani ya chumba cha mikutano kituo cha Kulea wazee na wasiojiweza cha Bukumbi Mwanza.
'Tumefika hapa kwasababu tumeguswa kwa aina mbalimbali kuleta kidogo tulichonacho ambacho kila mwanadamu hupenda kuishi, tutajitahidi katika zama zijazo, kuja na mbinu mbadala za mwendelezo wa kuwasaidia wazee hawa" Kisha akaongeza nawasihi vijana wenzangu tufanye kazi na kujiwekea akiba ya uzee ili tuwe na uwezo wa kujikimu kwa maisha ya baadae" katikati ya kusanyiko la kutoa msaada kwa Kituo cha wazee na wasiojiweza cha Bukumbi Mwanza, ni Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Daladala Kanda ya Ziwa Bw. Dede Petro
Tunafanya Haya Yote tukienzi mema aliyofanya BABA WA TAIFA MWL.NYERERE katika kusaidia Jamii isiyojiweza.
Wadau wa Taasisi ya Ki-Islaam ya UMU SALAAM ndani ya tukio.
Kuna changamoto nyingi zinazo wakabili wazee hawa, licha ya kukosa chakula kwa mpango sahihi wa lishe, afya duni na kukosa usaidizi kuna wengine hawawezi hata kujiogesha, kujilisha au hata kutoka nje ili wapate kuota jua kwaajili ya kushtua misuli ya miili yao. Ni jukumu letu sasa kama jamii kutafuta mbinu mbadala ili kusukuma angalau siku moja ya tabasamu kwa jamii hii ambayo ni kama imesahaulika. Tuwasaidie wazee wetu kwani kijana wa leo ndiye mzee wa kesho....
Picha ya pamoja na Afisa Ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza, wadau wa EPHC RURAL, METDO, wadau wa Taasisi ya Ki-Islaam ya UMU SALAAM, Kituo cha Soka cha Marsh Athletics Centre, na Jembe Fm.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.