ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 14, 2016

LIVERPOOL YAIDUNGUA ARSENAL NYUMBANI KWAKE 3 - 4, MOURINHO KWAKE KICHEKO.


Liverpool ilitoka nyuma na kufanikiwa kuilaza Arsenal katika mchuano mkali uliopigwa katika uwanja wa Emirates.
Theo walcot aliifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 31 mda mfupi baada ya kukosa mkwaju wa penalti.
Lakini Phillipe Coutinho alisawazisha kwa kufunga bao zuri kupitia mkwaju wa adhabu kabla ya Adam Lallana kufunga bao la pili mda mchache tu baada ya kipindi cha pili kuanza.
Coutinho alifunga bao la tatu na Sadio Mane akaongeza la nne kabla ya Alex Oxlaide Chamberlain kufunga bao zuri la pili naye Calum Chambers akafunga bao la tatu kwa kichwa.

MOURINHO AANZA VYEMA KIBARUA CHAKE MAN U.

KOCHA Jose Mourinho ameanza vyema harakati zake za kulisaka kombe la ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuishinda Bournemouth.
Juan Mata,ambaye alitolewa baada ya kuanza katika kombe la Community Shield alianza kufunga baada ya mchezaji wa Bournemouth Simon Francis kufanya masikhara.
Wayne Rooney alifunga bao la pili kwa kichwa kabla ya Zlatan Ibrahimovic kupata bao lake la kwanza akiwa na Manchester United kupitia mkwaju wa yadi 25.
Adam Smith aliifungia timu hiyo ya nyumbani bao la kufutia machozi.
United walicheza mechi hiyo bila Paul Pogba,huku kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan akicheza kama mchezaji wa ziada baada ya Mata kuanzishwa. 
CHANZO BBC SWAHILI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.