ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 23, 2015

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA IDD EL HAJI KWA MAKUNDI MBALIMBALI

 Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Mwakilishi wa Mahabusu ya Watoto Upanga, Regina Kuname msaada wa vyakula na kitoweo cha mbuzi na mafuta ya kula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya ya Idd El Haji Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Chama cha kulea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza, Hassan Hamisi kwa ajili ya sherehe hiyo.
 Mbuzi wakiingizwa kwenye gari baada ya wahusika kukabidhiwa.
 Vyakula vilivyotolewa na Rais Jakaya Kikwete vikiwa eneo la tukio vikisubiri kuchukuliwa.

Mwakilishi wa Kituo cha Wazee na Wasiojiweza cha Nunge kilichopo Kigamboni, David Mpangala akiwa na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya kituo hicho.


Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya vyakula na kitoweo kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji ambayo inaadhimishwa duniani kote leo.

Zawadi hiyo imekabidhiwa kwa makundi hayo kwa niaba yake na Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo Dar es Salaam leo asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Fungamo alisema Rais ametoa zawadi hiyo kwa ajili ya Sikukuu ya Idd El Haji kama anavyofanya siku zote wakati wa sikukuu mbalimbali.

Fungamo alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni Mahabusu ya Watoto ya Upanga iliyopo Manispaa ya Ilala, Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nunge, Kigamboni, Chuo cha Watu wenye Ulemavu cha Yombo Temeke na Kituo cha Kulelea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza.

Alitaja vituo vingine kuwa ni Kituo cha Makao ya Watoto Yatima cha Mburahati, Ilala, Kituo cha Makao ya Watoto-Kurasini, Kituo cha Full Gospel, Temeke na Kituo cha Watoto Alsaad Children House Kurasini.

Alivitaja vituo vingine kuwa ni cha Vosa Mission cha Kongowe, Temeke na Kituo cha Kijiji cha Furaha kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Fungamo alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo ya Idd El Haji kwa upande wa Zanzibar kuwa ni Kituo cha Mabaoni kilichopo Pemba na Makazi ya Wazee Sebleni yaliyopo Unguja.

Alitaja vituo vingine vilivyopo mikoani vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni kituo cha The Village of Home cha Dodoma, kituo cha Moyo Mmoja cha Bagamoyo mkoani Pwani, kituo cha watoto cha Tosamaganga kilichopo mkoani Iringa na Mahabusu ya Watoto Arusha na Tanga(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.