ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 23, 2015

WANANCHI WATAKIWA KUTODANGANYIKA NA VITU VIDOGO VIDOGO

Mgombea Ubunge wa jimbo la Arumeru magharibi
Gibson ole Meiseyeki.

Na Woinde Shizza,Arusha

Wananchi hapa nchini wametakiwa  kuacha masihara ya kutoa kura zao kwa kudanganya kwa kupewa sukari,pesa na khanga, vitambaa ili waweze uwapigia kura wanasiasa wanaowarubuni ili kuweza kupata nafasi za uongozi kuanzia ngazi za uraisi,ubunge na udiwani kwani wanakuwa wanapoteza haki zao.

Na endapo watatoa kura zao kwa kununuliwa na kutofanyiwa yale wanayoahidiwa na kupewa moyo badala yake viongozi hao wakisiasa pindi wapatapo nafasi hizo wanafanya yao na kuwaacha wananchi wakitaabika na hali ngumu ya maisha yale yale ambayo yamepitiwa na chaguzi mbalimbali na ahadi lukuki ambazo wanapewa na wagombea wa nafasi mbalimbali badala yake wabadili mtazamo wao kwa kuchagua viongozi waukawa hususan chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ili kuweza kuwaletea mabadiliko ya kweli nayaharaka.

Hayo yameelezwa na mgombea Ubunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson ole Meiseyeki wakati akinadi sera zake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya kijiji cha kiranyi  iliyoko kata ya kiranyi  katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha na kuhudhuliwa na maelfu ya wananchi katika viwanja hivyo.

Aidha ameongeza kuwa anaomba ridhaa kwa wananchi ili kuweza kumchagua na kuenda kuikomboa nchi na mwananchi wakawaida ili kuweza kumudu maisha ya hali ngumu ya sasa ili kuweza kuleta maendeleo kunazia ngazi ya kitongoji ,kata ,tarafa hadi taifa kwa lengo l kumkomboa mwananchi ili kuweza kujiletea maendeleo yake mwenyewe.

Hata hivyo alivitaji  viapaumbele vyake kuwa nikuleta maendeleo katika sekta ya elimu .miundombinu ya barabara ,sekta ya afya ,maji ili kuweza kuikomboa nchi na wananchi wake walioko.

Aidha aliongeza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa hospitali katika kata hiyo atawajengea na kuweza kujenga shule nzuri yenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kupambana na adui umaskini na maradhi na ujinga.

Sambamba na hilo atahakikisha anasimamia vyanzo vya mapato vinaongezeka kwa hali ya juu ili kuweza kuleta maendeleo ya haraka katika jimbo hadi Taifa kwa kushirikiana na mh,Raisi wake Edward Ngoyai Lowassa ikiwa nisehemu ajenda ya maendeleo ni sera ya chama na umoja wao.

Aidha aliongeza kuwa ajenda ya elimu ni vipaaumbele cha kwanza hadi tatu hali ambayo ukimpa mwananchi elimu anaweza kujikwamua na hali halisi ya ,maisha magumu yaliyoko sasa ambapo wanashindwa kumudu hali ngumu ilyoko sasa kwani chadema wamejipanga kweli kweli kuweza kuleta mabadiliko ya kweli kuanzia ngazi ya uraisi ,ubunge na udiwani.

Awali akimnadi  mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) John Seneu aliwataka wanachi kuchagua mafiga matatu (full suite)ili kuweza kuenda na kuleta mabadiliko ili kuweza kutobakwa na vyama vingine kwa kuwa na viti vingi katika kufanya na kuamua maamuzi mbalimbali ya maendeleo na ajenda katika vikao mbalimbali katika halmashauri,bunge na mabaraza ya
mawaziri.

Aliwataka   wapiga kura kuweza kutoogopa kufanya mabadiliko katika nafasi za kisiasa ili kuweza kuletewa mabadiliko chanya na ya haraka katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake mgombea udiwani Gibson ole Meiseyeki amewataka wananchi kuweza kumchagua jembe   ili kuweza kuwaondolea shida na changamoto zilizoko katika kata yao kwani hakuna mtu anavumilia shida na kupenda maisha magumu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.