Kulia ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahali ya binti wa Kaka yake kutoka kwa Mzee Samweli Chaha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
Na:George GB Pazzo
BAADHI ya Watu wamekuwa wakiita ni Zawadi inayotolewa kwa Wazazi ama Walezi pindi
binti anapokuwa katika mipango ya kuolewa. Lakini kwa umaarufu wake, watu wengi
wamekuwa wakiita Mahali.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na
majadiliano makali juu ya dhana halisi ya Mahali. Hoja mbalimbali zimekuwa
zikitolewa zikieleza kuwa suala la Mahali kwa sasa si muhimu sana kama
ilivyokuwa katika miaka ya zamani hususani kwa baadhi ya makabila nchini
ikiwemo kabila la Wakurya wanaopatikana Mkoani Mara ambapo wazee wa kabila hilo
walikuwa wakipokea mamia ya ng’ombe kama mahali pindi mabinti zao walipokuwa
katika mipango ya kuolewa.
"Kwa kabila la Wakurya bado suala la Mahali
lina umuhimu mkubwa japo kumekuwepo na mabadiliko kidogo. Zamani binti wa
kikurya alipokuwa akitaka kuolewa, Wazazi ama Walezi wake walikuwa wakipokea
mamia ama makumi ya ng’ombe kama sehemu ya mahali". Anaeleza mmoja wa
wazee Wilayani Tarime na kuongeza;
"Lakini hivi sasa hali haiko hivyo tena
kwani binti wa kikurya anaweza kuolewa kwa Mahali chini ya ng’ombe 10 ama pesa
kati ya Shilingi Laki Nne hadi Milioni Moja na Laki Tano hii ikitegemea nafasi
aliyo nayo binti. Mfano Mahali inaweza kupanda kama binti ni msomi, Mrembo ama
mwenye nidhamu na maadili mema katika jamii".
Miongoni mwa maoni yanayotolewa na baadhi ya
wanaharakati wa kutetea haki za binadamu yanakinzana na uhalali wa Mahali kwa
misingi kwamba suala la Mahali limekuwa halichukuliwi kama zawadi na watu wengi
na badala yake limekuwa likisababisha muoaji (Mme) kumnyanyasa muolewaji (Mke)
kwa minajili ya kwamba yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mkewe kwa kuwa
tayari anakuwa amemlipia mahali ambapo hatua hiyo huondoa dhana kuwa Mahali ni
zawadi na kugeuka kuwa kumtolea binti Mahali ni sawa na kumnunua ijapokuwa
dhana hii inapingwa sana na watu wengi.
Hata hivyo baadhi ya Wazee kutoka Kabila la
Wakurya Wilayani Tarime waliozungumza na Binagi Media Group wanaeleza kuwa bado
suala la Mahali lina umuhimu mkubwa sana hususani katika Kabila la hilo la
Wakurya na kwamba binti akitolewa mahali hueshimika katika jamii huku urafiki
baina ya pande zote mbili za familia kwa maana ya Mme na Mke ukiimarika zaidi.
Je wewe una mtazamo gani juu ya Mahali kwani
licha ya kuchukuliwa kama zawadi, baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa
kumtolea binti Mahali ni sawa na kumnunua. Wasiliana nasi kupitia nambari +255
(0) 757 43 26 94 au barua pepe binagimediagroup@gmail.com
Tazama picha za Sherehe ya Mahali ya Milika
Daniel Marwa Binagi Mzaliwa wa Kijiji cha Kenyamanyori kwa sasa akiishi Mtaa wa
Rebu ambae anatarajia kufunga ndoa na John Samwel Chacha Kebasa mkazi wa Mtaa
Rebu pia ikiwa ni Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Wa pili Kulia waliokaa ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahali ya fedha kwa ajili ya kumuoza binti wa Kaka yake aitwae Milika Daniel Marwa Binagi kutoka kwa Mzee Samweli Chacha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
Mahali Ikihesabiwa
Baada ya Mahali kukamilika hatua iliyofuata ni familia ya mme na mke kusaini mkataba wa Makubaliano chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
Mkataba ukisainiwa
Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi Mkataba wa Mahali na Mzee Maina (Kushoto) ikiwa ni upande wa binti
Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi Mkataba wa Mahali na Mzee Samwel Chacha Kebasa (Kushoto) ikiwa ni upande wa mme
Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
Wa kwanza kushoto waliosimama ndie Mkwe na hapo anatambulishwa Wazee
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Wazee upande wa binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya kuchukua Mahali kufikia tamati.
Hatimae wazee wakafika nyumbani na kufikisha habari njema kuwa Mahali imechukuliwa na hapa wakaweka kumbukumbu ambapo Kutoka Kushoto ni Mzee Maina Binagi, Milika Daniel Binagi na mwanae, Mzee Chacha Binagi, Leah Daniel Binagi pamoja na Professor Lloyd Binagi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.