Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai, 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney |
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot
amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa
kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba nchini Tanzania.
"Nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa
kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la nadra sana Barani
Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani namna hii" Bw. Abbot amemuambia Rais Kikwete na kumueleza awe na
uhakika kuwa " Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za
kuleta maendeleo na kukuza uchumi" ameongeza.
Rais Kikwete na Waziri Mkuu Abbot pia
wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana katika kulinda
usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na
kijamii.
Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko
rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter
Cosgrove.
Rais Kikwete amepokelewa leo asubuhi
tarehe 28 katika makao Makuu ya kiongozi wa Australia kwa
heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha mchana na
baadae kupanda mti kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya nchi hizi
mbili kwa kipindi kirefu kijacho.
Tanzania na Australia zimedumu katika
ushirikiano baina ya nchi zao tangu miaka ya sitini na sasa nchi mbili
hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya zaidi katika sekta mbalimbali
zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.
Baadae leo jioni Rais Kikwete atakutana na
wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania kwa
ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi
Tanzania inaweza kunufaika kutokana na kupata gesi.
Tayari Serikali ya Australia na makampuni
binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi
stadi VETA na tafiti mbalimbali katika Kilimo.
Kesho tarehe 29 Julai, 2015 Rais Kikwete
anatarajia kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu
cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha
miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.
Rais Kikwete anatarajia kuondoka Australia na
kurejea Tanzania baada ya shughuli ya kupokea shahada yake na ratiba yake kwa
ujumla.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Canberra-Australia
28 Julai, 2015
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.