ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 29, 2015

AIRTEL YATANGAZA WASHINDI WA DRAW YA PILI YA PROMOSHENI YA 'JIONGEZE NA MSHIKO'

Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.
Afisa Uhusiano na matukio wa wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akiongea na waandishi wa Habari katika droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akisikiliza (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.
Afisa Uhusiano na matukio wa wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akimsikiliza mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akifurahia nae  (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.

Airtel Yatangaza Washindi wa  Draw ya Pili ya Promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”

Dar Es Salaam, 28 July 2015, Airtel Tanzania leo imefanya droo yake ya Pili kwa wateja wake katika kampeni ijulikanayo kama “Jiongeze na Mshiko”. Kampeni hii ilianza rasmi tarehe 13 July 2015 na itaendelea hadi tarehe 10 Novemba 2015

Akiongea na waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki amesema; “kila wiki, droo hii itawapatia wateja wawili nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni tatu za kitanzania, mmoja shillingi milioni moja kila wiki na mwingine milioni tatu kila wiki.

Kwa wale watakaoingia katika droo ya milioni moja watajiunga na kushiriki bure na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milioni moja kila wiki na mwishoni mwa droo hii kuweza kujishindia shilling milioni 2. Na kwa wale washindi wa wa milioni tatu, mteja anaweza kuamua kuingia na kushiriki kwa tozo ya shilingi 300 kwa siku na mwisho wa promosheni mteja ataweza kujishindia milioni 50.

Akitangaza washindi Dangio alisema" Leo tumechezesha droo ya wiki ya
pili tangu kuzinduliwa kwa promosheni ya ”Jiongeze na Mshiko" wiki
mbili zilizopita. Ninayo furaha kutangaza washindi hao ambao ni
Gabriel Fernandis(18) mwanafunzi na mkazi wa wa Mkoa wa Musoma Mara yeye amejishindi shilingi milioni 1 , na  mshindi wa pili ni Hamis Rashid(52)na mkazi wa mkoa waTabora Sikinge yeye amejishindi shilingi milioni 3.

“Ushiriki upo wazi kwa wateja wote wa malipo ya awali. Wanachotakiwa kufanya ni kujiunga na promosheni hii  kwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.