![]() |
Bw. Ramia Mazwela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Bodaboda wa Kanda yaTabata, akizungumza na waandishi wa habari namna alivyo upokea kwa furaha utaratibu huo. |
![]() |
Waendesha bodaboda wa Kanda ya Tabata wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa zoezi la kugawiwa sare (Reflactors) kwaajili ya utambuzi. |
KATIKA hali ya kukabiliana na changamoto nyingi kwenye sekta ya bodaboda kampuni ya mawasiliano na matangazo ya
Alternative Communication yajijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya
Vodacom TanzanianaJeshi la Polisi wametengeneza mfumo salama wa kumbukumbu kwa waendesha bodaboda ili kuwasaidia bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.
Hatua hiyo inakuja kufuatia madai kuwa baadhi ya waendesha bodaboda wasio kuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu
au kutumiwa na wahalifu kuvunja Amani na kupotea bila ya kutambulika.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.
Edward Mgaya amesema jijini Dar es Salaam kwamba tayari kampuni hiyo imekwisha wasajili bodaboda
3,000 katika mfumo huo.
Ameongeza kwamba wale waliosajili wapi awatapatafaida ya kupewa huduma ya bima,
mafunzo ya usalama barabarani na Ujasiriamali.
Bw.
Mgaya alisema wale wanaosajiliwa katika mfumo huo wanapewa koti (Reflectors) zilizo na namba ya usajili mbele na nyuma ya koti,
Namba hiyo ni utambulisho kamili wa mwendesha pikipikipi akwenye kofia zao(helmet)
itabandikwa namba ya simu ya Kiongozi wa Chama cha Waendesha Bodaboda husika.
“Mtu yoyote akiipiga namba ya chama
cha waendesha bodaboda na akataja namba ya usajili wadereva wa bodaboda,
mfumo utamtambua dereva huyo mara moja.
Bw.
Ramia Mazwela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Bodaboda wa Kanda yaTabata,
ameelezea kufurahishwa na utaratibu huo mpya wenye faida kubwa kwao,
na kwamba mfumo huo utaboresha usalama katika eneo lake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.